"Baada Ya Dhiki Kuu" movie kamili na Kiswahili Subtitles
Watch Video
October 2, 2015
Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa;
na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake;
lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo. " - Ezekieli 33:6
Asubuhi na mapema Jumanne hii ya tarehe September 11, 2001
-Al, ni asubuhi njema, sivyo? - Ni asubuhi kamili ya majira ya majani kupukutika.
Siku ya Septemba , , dunia ilibadilika. .,
"Nchi ya Walio Huru" sasa imekuwa
nchi ya watwana. Watu wa taifa lilipata kutukuka la
Marekani wameuza uhuru wao ili kupata usalama.
Lakini haya yote yalikuwa yamepangwa?
"Disemba , , ni tarehe ambayo haitasahaulika.
Nchi ya Marekani ilishambuliwa ghafla na kwa makusudi.
Maswali mengi bado yapo kuhusu matukio ya siku hiyo
inayokumbukwa kwa mabaya. Lakini jambo moja
tulijualo kwa hakika: shambulizi la kustukiza la
Pearl Harbor ilianzisha mfululizo wa matukio.
ambayo hatimaye yatafufikisha kwenye
Serikali Moja ya Dunia.
"Japani ilianzisha vita hivi kwa uchimvi.
Tutaimaliza kwa ushindi."
Baada tu ya vita kuu ya pili ya dunia
Umoja wa mataifa ulianzishwa na safari kuelekea
serikali moja ya dunia ikashika kasi. Kila vita
inatusogeza hatua moja karibu na kile Biblia inakiita
"mwisho wa dunia." Alama
zinawekwa kila mahali; serikali katili
inazidisha udhibiti wa wananchi wa
Marekani, na kwa wale wanaoelewa
unabii wa Kibiblia, kitakachofuata
hakitawashangaza.
Muda fulani baadaye, Biblia inasema
kwamba kila mtu hapa duniani
atatakiwa kupokea chapa ili aweze kununua
au kuuza. Wakati mfumo wa sasa wa uchumi unaanguka,
na kadiri teknolojia inavyoongezeka, pesa taslimu zinakuwa
zimepitwa na wakati. Na uhalisia wa
jamii isiyotumia pesa hauko mbali sana. Hakika, tayari imeanza
kutekelezwa. Licha ya wengi wasioamini
viongozi wa dini, watu waovu hawalali
wakipanga kuleta Mfumo Mpya wa Dunia.
Tunaweza kuuona mwisho ukikaribia haraka, na
mazingira yakiandaliwa ili MpingaKristo atokee.
Tunaweza kusikia sauti za wale wanaovunja
katiba yetu ya Marekani
na kuhamasisha mfumo huu mpya wa serikali ya dunia
".... a new world order..."
Na hayo yakikaribia kabisa,
filamu hii inazidi kuwa muhimu sana.
Shetani anafanya kazi kimyakimya kuleta
serikali moja na dini moja duniani
ili kumwandaa mpingakristo. Na pia
amewadanganya wakristo wengi wa siku hizi
waamini kwamba wataondolewa duniani
kabla ya Dhiki Kuu haijaanza.
Mafundisho haya yajulikanayo kama "unyakuo kabla ya dhiki kuu"
yanadai kwamba Kristo atarudi wakati wowote,
na kwamba hakutakuwa na ishara yoyote
ya yeye kurudi. Matokeo ya uongo huu,
Wakristo wengi hawajajiandaa kabisa
kwa yale Biblia iliyotuonya yanakaribia kutokea.
Ingawa maandiko yanasema wazi kwenye Matayo
, na kwengineko, kwamba unyakuo utatokea
BAADA YA DHIKI KUU, wahubiri wakbuwa,
vyuo vya Biblia, na sinema mashuhuri
kama ile ya Left Behind zimewafundisha wengi kutarajia
unyakuo kutokea muda wowote.
Na kwa vile Wakristo karibu wote hawajajisomea
Biblia yote, wachache wanaelewa
kwamba unyakuo-kabla-ya-dhiki-kuu ni uzushi
nje ya maandiko. Lakini kama unyakuo kabla ya dhiki
Lakini kama unyakuo kabla ya dhiki kuu hautokani na maandiko, unatoka wapi basi?
Baada ya Dhiki Kuu
Jina langu ni Steven Anderson,|N na ni Mchungaji wa Kanisa la Kibaptist la Faithful Word
lililoko Tempe, Arizona, na niko kwenye kazi
ya kuelimisha watu kuhusu unyakuo kabla ya dhiki kuu
kwa vile ni mtazamo unaotokana na
kutofahamu, na ninaamini kwamba kama
watu watayaona maandiko na ukweli
haitakuwa vigumu kwao
kubaini kwamba unyakuo
utakuja BAADA YA DHIKI KUU.
Jina langu ni Roger Jimenez.
ni mchungaji wa kanisa la Kibaptisti Verity huko Sacramento, California.
Nilikulia kwenye familia ya Kikristo
na nilifundishwa kuamini unyakuo-kabla-ya-dhiki
maisha yangu yote, na sikuwa kuwa na sababu
ya kutilia mashaka. Wahubiri walituambia hayo, na
nami niliipokea kama ilivyo, lakini
kadiri nilivyozidi kufundishwa hayo, nilianza
kuona ilivyo mbali na maandiko,
na naona hitaji la kufundisha
Biblia na kuuweka wazi ukweli.
Mch. Anderson: unyakuo kabla ya dhiki
ni mafundisho mapya. Hakuna ushahidi
wa mafundisho hayo kabla ya mwaka .
Mch. Jimenez: Tuelewe kwamba mwaka
ni karibu sana kihistoria. Kwa maelfu
ya miaka toka wakati wa Kristo, tumepitia mageuzi, tumepitia
watheolojia mbalimbali - ukikubaliana au la
na watu kama Martin Luther, au
John Calvin, au yoyote, ukweli ni kwamba
maelfu ya vitabu, maelfu ya machapisho, maelfu
ya insha, na mahubiri lukuki
yamefanywa kabla ya ,
Mch. Anderson: Ninachosema ni
hakuna ushahidi wa yoyote toka dhehebu lolote,
la Kikristo, ambaye amefundisha
haya mafundisho.
Mch. Jimenez: Unapoangalia historia
inabidi ujiulize
"Nini chanzo cha mafundisho ya
unyakuo-kabla-ya-dhiki?"
Dk. Roland Rasmussen: Moja ya washabiki wa
unyakuo-kabla-ya-dhiki ni mtu aitwaye
John Nelson Darby. Mnamo miaka ya , alianza
kufundisha kile alichokiita
"Unyakuo wa Siri". Baadaye alitengeneza tafsiri yake
mwenyewe ya Biblia ambayo
aliondosha mistari mizima, akichakachua mafundisho
muhimu ya Biblia, na kuvuruga
vifungu muhimu vihusuvyo kurudi kwa Yesu Kristo.
John Nelson Darby, ajulikanaye kama "Baba wa
Mafundisho ya Nyakati Mamboleo," akitangaza
nadharia ya unyakuo kabla ya dhiki
muda wote wa karne ya . Baadaye, unyakuo kabla
ya dhiki ulisambaa na kukubaliwa miongoni
mwa Wabaptisti wakati Oxford University Press ilipochapisha
Biblia toleo la Scorefield Reference iliyokuwa na
maelezo pembeni yakitangaza mawazo ya Darby ya
unyakuo wa siri. Maelezo hayo yamesababisha
Wakristo wengi wapokee mafundisho hayo kana kwamba
Mungu mwenyewe ndiye aliyeyasema.
Mch. Anderson: Ibilisi ametumia hii zana ya
Maelezo ya Ziada ya Scorefield kwenye Biblia
kuliko zana yoyote katika kusambaza mafundisho haya
ya unyakuo kabla ya dhiki. Wajua kwamba
imetoka wapi? Hivi ndivyo yalivyoingia kwenye makanisa.
Hapa ndipo wachungaji wanapoyatoa.
Haitoki kwenye Biblia. Bayana
haikutoka kwenye kinywa cha Yesu Kristo!
Lakini kilitoka kwenye mdomo wa Scofield. Maelezo
ya Scofield yaliasisi unyakuo kabla ya dhiki,
na yalimfanya msomaji aamini kwamba ni
yanatokana na maandiko wakati sivyo
kabisa. Kwa vile Biblia ya Scofield inatumiwa
na seminari nyingi na vyuo,
na pia wahubiri wengi vijana hutumia Biblia ya
Scofield, walianza
kuchukulia unyakuo kabla ya dhiki kana kwamba
ni ukweli na kuanza kuuhubiri.
Dk. Roland Rasmussen: Uchakachuaji wa
unyakuo wakati wowote ulifika hadi kwa kizazi cha miaka ya sabini
kupitia kwa filamu za Don Thompson.
"Ghafla na bila taarifa, maelfu mengi, pengine mamilioni ya watu walipotea ghafla.
Maelezo ya mashuhuda wachache wa kupotea huku hawaelewa,
Lakini jambo moja ni la hakika. Mamilioni waliokuwa jana usiku wakiishi duniani humu hawapo hapa asubuhi hii.
Dk. Roland Rasmussen: Filamu tatu za Thompson
Zilifanya kazi kubwa kuwapumbaza
kizazi kipya cha vijana. Tangu izinduliwe zaidi ya
watu milioni wameona filamu ya "A Thief in the Night"
Mwaka , Tim Dalehouse alichapisha kitabu cha simulizi la mwisho wa Dunia "Left Behind" cha Tim LaHaye na Jerry Jenkins.
Mch. Anderson: Huu ni mfululizo wa hadithi
zinazoonyesha kila mtu hajulikani alipo na hakuna mtu
ajuaye waliko. Magari yanagongana;
ndege zinaanguka kwa vile
rubani amekwenda, na masimulizi haya ya kusisimua
ya unyakuo kabla ya dhiki yamekuwa
sehemu ya utamaduni wa Kimarekani, na watu
wameyapokea tu kama vile ni kweli, na ...eh...
Ni filamu ya kijinga.
Dr. Roland Rasmussen: Hatimaye filamu ya
Left Behind iliuza nakala milioni duniani kote,
ikifuatiwa na mfululizo wa vitabu , na matoleo ya
mengine matatu mpaka sasa. Lakini Left Behind ni
kazi ya usanii. Ili kujua ukweli kuhusu unyakuo
inabidi tusome Biblia yenyewe.
Mch. Anderson: Thesalonike
ni maandiko ya unyakuo.
Na katika Thesalonike Sura ya , tunaona
maandiko mashuhuri pengine kuliko yote kuhusu unyakuo.
Mch. Anderson: Kila mtu atakubali kwamba
maandiko haya yanazungumzia unyakuo. Haya
ni mafundisho bayana kuliko yote kwenye Biblia yafundishayo
kuhusu Yesu kuja mawinguni, nasi
kwenda kumlaki. Biblia inasema kwenye
mstari wa :
( Wathesalonike :): " Lakini, ndugu, hatutaki
msijue habari zao
waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na
wengine wasio na matumaini. "
( Wathesalonike :) "Maana, ikiwa twaamini
ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao
waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja
naye.
Mch. Anderson: Hivyo, asemacho hapa ni kwamba
hataki wawe wasiojua
kuhusu Wakristo, waamini waliokufa,
ambao wamelala katika Yesu, wale ambao tayari
wameshaenda kukaa na Bwana. Anasema,
Hatutaki msijue habari zao waliolala
msije mkahuzunika kama na wengine wasio na
matumaini. Nataka mjue kwamba
mtawaona tena wapendwa waliokuwa
wameokoka. Mtawaona tena
kwa vile Biblia inasema kwamba wakati
Yesu Kristo anarudi tena, atawaleta
pamoja naye. Waliokufa katika Kristo watafufuka/N kwanza, na kadhalika. Ndiyo maana alisema kwenye mstari wa
( Wathesalonike :) Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Mch. Anderson: Ndiyo maana andiko hili ni
hupendwa sana kutumiwa kwenye misiba.
Nimekuwepo kwenye misiba mingi ambayo watu
hutumia maandiko haya kufarijiana.
Kwa hiyo katika kila mstari, anazungumzia ukweli kwamba tutawaona tena watu waliokwisha kufa.
( Wathesalonike :) Kwa kuwa twawaambieni
haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi
tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake
Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
( Wathesalonike :) Kwa sababu Bwana
mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,
na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;
nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
( Wathesalonike : ) Kisha sisi tulio hai,
tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja
nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani;
na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
(Wathesalonike :) Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Mch. Anderson: Kwa hiyo ukiuelewa muktadha,
faraja ni kwamba tutawaona wapendwa
wetu tena. Anasema, Mtawaona tena
kwa vile kama mkiamini Yesu alikufa na
akafufuka, vivyo hivyo (vilevile), na wao waliolala mauti katika Yesu Mungu atawaleta pamoja naye.
Watafufuliwa. Waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza,. Anasema,
Farijianeni kwa maneno haya. Hakuna
faraja isemwayo hapa kwamba
mtaepuka dhiki. Hamtateswa.
Hamtapitia
dhiki kuu. Hamtapitia mateso.
Hamtapata adha. Kwani
vifungu hivi hata vinataja dhiki kuu?
Pana chochote cha dhiki kuu kilichoongelewa?
Hapana. Hakusema, Farijianeni kwamba
hamtapitia dhiki kuu. Farijianeni
kwamba hamtateswa. Farijianeni kwamba
kabla ya dhiki kuu pana
unyakuo. Hayo siyo asemayo!
Mch. Jimenez: Sasa tusomapo vifungu hivi,
pana tabia chache tunazoweza
kubaini kuhusu unyakuo ambazo zitatusaidia
kubaini unyakuo katika vifungu vingine. Ningependa
Uelewe kwamba unyakuo una vitu gani.
Kama ukiusoma mstari ule wa ,
unasema, "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka
kutoka mbinguni..." Hivyo jambo la kwanza la
kuelewa kuhusu unyakuo ni kwamba
Bwana atashuka toka mbinguni na mwaliko
na sauti ya malaika mkuu, na nataka uzingatie haya
"na
parapanda ya Mungu." Hiyo ni tabia ya pili
ninayotaka ufahamu kuhusu unyakuo.
Bwana atashuka, patakuwa na parapanda ya
Mungu, na kisha Biblia inasema, "Wafu
katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tuta..." Zingatia
maneno haya: "tutanyakuliwa pamoja nao katika/N mawingu..." Hivyo wakati unyakuo unatokea,
Kwa mujibu wa Wathesalonike sura ya ,
sifa za unyakuo ni:
. Bwana atashuka . Parapanda italia .
Tutanyakuliwa mawinguni
Mch. Jimenez: Tutanyakuliwa tukamlaki mawinguni.
Mch. Anderson: Rudi kwenye Mathayo na
utaona sifa hizihizi kwenye Mathayo :-.
Ona Mathayo :,"Lakini mara, baada ya
dhiki ya siku zile, "
Nataka kuwauliza watu, "Ni sehemu ipi ya BAADA
msiyoielewa kuhusu andiko hili?"
Lakini linasema:
(Mathayo :)Lakini mara, baada ya dhiki ya
siku zile, jua litatiwa giza, na
mwezi hautatoa mwanga wake, na
nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu
za mbinguni zitatikisika;
(Mathayo :) ndipo itakapoonekana
ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo
mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao
watamwona Mwana wa Adamu ["Mwana wa
"Adamu ni jina alilojiita Yesu mwenyewe
alipokuwapo duniani] akija
juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
(Mathayo :) Naye atawatuma malaika zake
pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao
watawakusanya wateule wake toka pepo nne,
toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Mch. Anderson: Sifa zote! Yesu
kuja mawinguni. Sauti ya parapanda.
Anawatuma malaika kuwakusanya wateule wake.
Mch. Jimenez: Sababu nimekuonyesha haya
ni kwamba nataka uelewe kwamba kwenye
Mathayo :-, tunaona unyakuo, na
tukiulinganisha na Wathesalonike :-,
vinashabihiana kikamilifu.
Mch. Anderson: Usifunge hapo, nenda Marko .
Marko kimsingi inasema
vitu vilevile Mathayo inavyovisema. Ni kile
ambacho tunaweza kukiita "vifungu sambamba".
Utaona mahubiri yaleyale, mafundisho yaleyale
kwenye sura hizi mbili. Unaweza kuziweka
upande kwa upande. Zinasema vitu vilevile. Acha
nikuonyeshe sura hiyo. Inasema
mstari wa :
(marko :) Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo,
jua litatiwa giza, na
mwezi hatautoa mwanga wake.
(Marko :) na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.
(Marko :) Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.
(Marko :) Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka
pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.
Mch. Anderson: Mpaka hapa tunaweza tu
kuomba na kurudi nyumbani. Tungeweza tu
kufunga Biblia yetu, na kusema, "Ndiyo hivyo,
jamani. Ni BAADA YA DHIKI KUU," na
kufunga tu Biblia zetu na kwenda nyumbani. Lakini ah
hatutafunga Biblia zetu hivi na
kwenda nyumbani kwa vile nitakuthibitishia
na kukuonesha kwamba haya yanazungumzia
unyakuo, na yanasema kwamba ni BAADA YA
DHIKI KUU.
Mch. Anderson: Watu wengi watapinga
sura hii na kusema, "Huwezi kupata
mafundisho yako toka Mathayo kwa vile Mathayo
anazungumza tu na Wayahudi.
Watapuuzia vifungu hivi, na kusema, "Aah,
haya ni kwa ajili ya Wayahudi pekee." na mwanazuoni
fulani alishaamua kwamba kitabu cha Mathayo
ni kwa ajili ya Wayahudi, kitabu cha Marko ni kwa
Warumi, kitabu cha Luka ni kwa Wayunani,
na kitabu cha Yona ni kwa ulimwengu. Ah
Asante Mungu kwa kutukumbuka walau
kwenye moja ya injili nne! Lakini ni nani aliyebuni
maneno haya? Pengine Mathayo alielemea kwa
Wayahudi. Huenda Luka alielemea kwa
Wayunani. Labda waraka wa Paulo kwa Waefeso
ulikusudiwa kwa Waefeso. Unaonaje?
Labda waraka wa Paulo kwa Waebrania ulikusudiwa
kwa Waebrania. Pengine waraka
wa Paulo kwa Wathesalonike uliwalenga
Wathesalonike, lakini kila ahadi kwenye
Biblia ni yangu! Kila sura, kila kifungu, kila mstari,
Kitabu cha Tito hakikuwa
kwa Tito pekee! Hicho kilikuwa ni kitabu
cha muda mfupi! Ni kwa kila mchungaji kukisoma. Ni kwa kila
mwamini kukisoma. Ni Agano Jipya!
Mch. Anderson: Lakini watasema hivi
|Hapana, Mch. Anderson, we huelewi tu."
Mahubiri haya yote yalihubiriwa kuhusu Wayahudi,
kwa Wayahudi, kwa ajili ya Wayahudi. Yesu Kristo
alikuwa akiwahubiri Wayahudi katika Mahubiri ya Mzeituni
(jina zuri la kitheolojia waliovipa
vifungu hivi). Mch. Anderson, alikuwa anazungumza
kwa Wayahudi! Huelewi! Aliposema
anaposema kwenye Marko :, Baada ya dhiki kuu, na
kisha akaongelea Yesu kurudi mawinguni
katika mstari wa , na kuwakusanya wateule katika
mstari wa , kutoka mwisho wa nchi,
mpaka miisho ya mbingu, hapo haongei tu
na Wayahudi." Sawa, angalia
mstari wa mwisho wa Marko : Na hilo niwaambialo
ninyi,Nawaambia wote. Usiache
mhubiri yoyote kujaribu kukwambia kwamba haya
ni ya Wayahudi tu. Si ya waamini wote.
Ndivyo isemavyo Marko :? Hapana! Inasema:
(Marko :) Na hilo niwaambialo ninyi nawaambia
nyote, Kesheni.
Mch. Anderson: Hilo ndilo neno la mwisho la
sura hii.
(Marko :) Na hilo niwaambialo ninyi,
nawaambia wote, Kesheni.
Mch. Anderson: Na bado watu watageuka na
kusema, "Sura hii
haizungumzi na wote. Inazungumza to na
Wayahudi." Ni kama alijua kwamba watu
watakachokuja kusema, kwa hiyo akasema hivyo
mwishoni. Siongei nanyi tu. Naongea
na wote nisemapo, Kesheni. Hili ni kwa kila mtu.\Kusema kwamba sura hii anaongea
tu na Wayahudi ni kichekesho kwani bayana anasema:
(Marko :) Na hilo niwaambialo ninyi,
nawaambia wote, Kesheni.
Mch. Jimenez: Mara nyingi watu huangalia
Mathayo:-, na kusema, "Sawa,
hata kama inaonekana ni kama unyakuo, na
hata kama inasikika kama unyakuo, lakini
siyo unyakuo," na hii ndiyo sababu watoayo
kusema siyo unyakuo.
Ukiutazama mstari wa , unasema, "Naye
atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya
parapanda, nao watawakusanya wateule wake..."
na watu watatazama hilo
andiko, na kusema, "Unaona? neno ni
'wateule' siyo Wakristo." Watasema,
"Hao 'wateule' ni Izraeli. Kwa hiyo Mathayo
siyo unyakuo. Haikukusudiwa
kwa Wakristo. Sura hii nzima imekusudiwa
Wayahudi kwa vile anaongelea wateule."
Muhimu hapa ni hili: mara zote tuiachie
Biblia iwe ni kamusi yake yenyewe.
Mch. Anderson: Ninayo hapa orodha ya kila mara
neno 'wateule' limetumika.
Hatutaisoma yote kwa vile muda hautoshi
,lakini ningeweza kupitia kila mara "wateule"
limetumika, na ningeweza kukuonyesha kwamba kila
wakati, linazungumzia watu ambao
Mch. Jimenez: "Sababu ambayo watu hufikiri neno "wateule" lina maana ya "Wayahudi", au linazungumzia
"Izraeli" ni kwamba badala ya kujifunza Biblia,
na badala ya kusoma Biblia
wamekuwa wakisoma maoni, na wamekuwa
wakisoma vitabu vilivyoandikwa na watu, na
watu hao wamewaambia kwamba tafsiri ya neno
"wateule" ni ipi. Biblia ya Scofield
ina maoni kwenye Mathayo ikisema kwamba neno
"wateule" linamaanisha "Izraeli." Lakini
Biblia inajifafanua yenyewe, na Biblia inatupa
majibu kwa maswali yote ya mafundisho
tuliyonayo, na neno "wateule", ukilichunguza
kwenye Biblia yote, ni wazi siyo Wayahudi.
Mch. Anderson: Kukupa mfano rahisi, katika
Wathesalonike:, inasema:
( Wathesalonike :) Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;
Mch. Anderson: ...anazungumza na Wathesalonike ambao ni wazi walikuwa Mataifa. Tunaona kwenye Warumi
(Warumi :) Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
Mch. Anderson: Katika mara zinazotaja neno
"wateule" kwenye Biblia, nimeona mara zina maana
waamini wote kwa ujumla, mara mbili zinamaanisha
waamini ambao ni Mataifa,
mara moja inamaanisha waamini ambao ni Wayahudi
mara mbili zinamaanisha Yesu Kristo mwenyewe,
na mara moja inamaanisha Yakobo, mtu mmoja,
kuwa ni mteule wa Mungu. Nitakupa mstari
mmoja unaoonyesha wazi kwamba wateule haina
maana "Izraeli" kwa vile watu watasema,
wateule? Hao ni Izraeli. Hao ni Wayahudi."
(Warumi :) Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa
walikipata, na wengine walitiwa uzito.
Mch. Anderson: Kwa hiyo Biblia inasema, Izraeli
hakupata uteule. Sasa, kama Izraeli
walikuwa ndio wateule, hayo maandiko yasingekuwa
na maana yoyote.
Mch. Jimenez: Kwenye maandiko yote ni wazi,
ukiipa Biblia nafasi ya kufafanua
kwamba "wateule" siyo Wayahudi,
na kwamba "wateule" siyo taifa la Izraeli,
wateule ni waamini. Wanaweza kuwa wametokea
Asia ndogo; wanaweza kuwa Wayunani;wanaweza
kuwa mabedui; wanaweza kuwa wowote. Ukimvaa
Kristo, umevaa
utu mpya, na unahesabiwa kuwa mteule. Hivyo
tukirui kwenye Mathayo , na anaposema
"Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya
wateule wake," inaenda vizuri kabisa na vifungu, vinavyoonyesha ukweli kwamba ni unyakuo wa waaminio.
Mch. Anderson: Haihusiani kabisa na iwapo ni
Wayahudi au Mataifa, weusi
au weupe. Wateule ni wale waliookolewa.
Atawakusanya mawinguni
pamoja naye. Hiyo si ni sawa na isemavyo
Wathesalonike sura
ya ? Pale iliposema kwamba patakuwa na\Parapanda, na kwamba waamini watakuwa
wamenyakuliwa wawe pamoja na Kristo. Baadaye kidogo
kwenye sura hiyohiyo, inasema,"Walakini
habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye..." hivyo hakuna
ajuaye siku wala saa haya yatakapotukia.
Siwezi kukuambia, "Yatatokea mnamo Oktoba
xx ya mwaka huu." Tena, baadaye kido, anasema:
(Mathayo :) Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni;
mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
(Mathayo :) wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa,
mmoja aachwa.
(Mathayo :) Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
Mch. Anderson: Kwa hiyo Mungu anatuambia kwamba
hatujui ni lini itatokea. Itakuwa ni kitu
cha kutazamia. Hatujui siku wala
saa, lakini antuambia kwamba ni BAADA
YA DHIKI KUU kwa sababu alisema BAADA
YA DHIKI KUU jua na mwezi vitatiwa giza
na Yesu Kristo atarudi mawinguni. Hivyo
wakati parapanda inalia. Yaani wakati
waamini wananyakuliwa. Kwa hiyo kwa kuwa tu hatujui
siku wala saa, haina
maana kwamba ni jambo ambalo linaweza kutokea
muda wowote. Watu wengi huangalia
andiko "hakuna mtu ajuaye siku wala saa,"
na kusema, "Inaweza kutokea muda wowote."
Lakini, alikuwa punde tu ametoka kusema itakuwa BAADA
YA DHIKI. Haya yanapatikana
kwenye Mathayo, Marko na Luka. Mathayo ameyaweka
sura ya , Marko kwenye sura ya ,
Luka anayaandika katika sura ya na sura ya
na kisha Yohana anayazungumzia katika Ufunuo.
Yameandikwa na wote wanne. Kwanza inakuja
dhiki kuu, kisha jua na mwezi zatiwa giza,
kisha Yesu anakuja mawinguni katika unyakuo.
Mch. Anderson: Sababu inayowafanya watu wadhani
unyakuo ni kabla ya dhiki kuu
ni kwamba wanashindwa kutofautisha dhiki kuu na
ghadhabu ya Mungu. Namna moja ya kuthibitisha kwamba ghadhabu ya Mungu
na dhiki kuu ni vitu viwili tofauti
ni katika Mathayo:, inasema,
Lakini mara, BAADA YA DHIKI ya siku zile,
jua litatiwa giza, na mwezi
hautatoa mwanga wake." Hivyo Biblia iko wazi kabisa
katika Mathayo kwamba jua na
mwezi vitatiwa giza BAADA YA DHIKI. Hivyo,
ukienda kwenye Ufunuo utasoma
kuhusu jua na mwezi kutiwa giza (wakati muhuri
wa sita ukifunguliwa), Biblia inasema, "...na
jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu"
...sawa kabisa na ilivyosema katika Mathayo ...
(Ufunuo :) na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake,
utikiswapo na upepo mwingi.
(Ufunuo :) Mbingu zikaondolewa
kama ukurasa ulivyokunjwa, na
kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka
mahali pake.
(Ufunuo :) Na wafalme wa dunia, na
wakuu, na majemadari, na matajiri, na
wenye nguvu, na kila mtumwa, na
mwungwana, wakajificha
katika pango na chini ya miamba ya milima,
(Ufunuo :)wakiiambia milima
na miamba, Tuangukieni, tusitirini,
mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi,
na hasira ya Mwana-Kondoo.
(Ufunuo :)Kwa maana siku iliyo kuu, ya
hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Mch. Anderson: Hivyo, kwa mujibu wa haya, pale
lini hasira ya Mungu itashushwa? Pale
jua na mwezi vitiwapo giza ni pale wasemapo
"Siku ya ghadhabu yake imekuja."
Kauli ya IMEkuja, inamaanisha muda si mrefu.
Kwa hiyo Mathayo inasema kwamba jua na
mwezi vitatiwa giza BAADA YA DHIKI na
kama hasira ya Mungu haiji mpaka baada ya
jua na mwezi kutiwa giza, vinawezaje vyote kuwa
ni kitu kilele? Hivyo hukumu ya Mungu haiji
Mpaka jua na mwezi vitiwe giza.
Kwa kawaida ukiwauliza watu waonyeshe
maandiko yasemayo unyakuo utatokea kabla ya dhiki,
awawezi kukuonyesha andiko lolote. Nitawapa changamoto
mtu yoyote anionyeshe mstari mmoja ambao hasa
unatumia neno "dhiki" kuthibitisha
msimamo wao wa unyakuo kabla ya dhiki.
Hawawezi. Lazima wakuonyeshe mstari unaosema
neno "ghadhabu." Wataonyesha mistari inayosema
kwamba sisi Wakristo hatuko chini ya
ghadhabu ya Mungu, na wataonyesha vifungu visemavyo
kwamba hatuko chini ya ghadhabu, na
kwamba tumeokolewa toka kwenye hukumu. Na hapo
watasema, "Unaona? hapa, Biblia inasema kwamba
hatutapitia dhiki kuu. Lakini hebu ngoja:
dhiki kuu na ghadhabu ni vitu viwili tofauti!
Hakuna mstari ambao anayeamini unyakuo kabla
ya dhiki anaweza kukuonyesha unaotumia neno "dhiki"
ndani yake ili kukuthibitishia mafundisho yao. Watakuonyesha
mistari fulani juu ya ghadhabu ya Mungu. Lakini
ghadhabu ya Mungu na dhiki kuu ni vitu viwili
tofauti kabisa. Wakristo wengi wamefundishwa
makanisani mwao na vitavu wasomavyo
kwamba vitu hivi viwili ni kitu kilekile.
Na unapojaribu kuwaambia, "Ninyi!, Tutakuwepo hapa
wakati wa dhiki kuu!
Unyakuo hauji mpaka BAADA YA DHIKI KUU.
Haya ndiyo watajaribu kukuambia: "Hapana, Mungu
hawezi kushusha ghadhabu yake kwa watu wake mwenyewe.
Hatuko chini ya hukumu. Tutakuwa
mbali na ghadhabu yake." Hebu fikiria:
Ghadhabu ya Mungu na dhiki kuu ni kitu kilekile?
Hapana. Kwa hiyo, kama tukiweza kuwaelewesha watu
maana ya neno "dhiki", wangeweza
kuelewa kwamba unyakuo unakuja BAADA YA
DHIKI KUU. Ni vile tu watu
hawaelewi neno "dhiki" kwa sababu
wana fikra hizi vichwani mwao kwamba
dhiki ni miaka saba ambayo Mungu
atamimina ghadhabu yake na kumimina moto
na kiberiti, akibadili maji kuwa damu, na
kuwatesa watu kwa nge, na
mapigo mbalimbali. Sivyo ilivyo dhiki kuu.
Sivyo Biblia inavyofundisha.
Mch. Anderson: Wale waaminio kwenye kile
kinachoitwa "unyakuo bila dhiki", au unyakuo
unaokuja kabla ya dhiki kuu, kwamba unyakuo
unaweza kutokea muda wowote: hebu tuchambue
"unyakuo kabla ya dhiki." Ina vitu vitatu ndani yake
"Kabla".
"Dhiki" inasimama badala ya "dhiki kuu". Na kisha
una neno "unyakuo". Neno "unyakuo" haliko
kwenye Biblia. Dhana ya unyakuo iko kwenye
Biblia kwa vile tunasoma Yesu atakuja
na mawingu, na watu watanyakuliwa kwenda
pamoja naye hewani, n.k. Hivyo dhana ya
unyakuo iko hapo, lakini neno "unyakuo" haliko.
Je, neno "dhiki" lipo
Kwenye Biblia? Ukitafuta kila mstari unaotumia
neno "dhiki", limetumiwa mara
kwenye Agano Jipya. Hivyo kama Agano Jipya
linatumia neno "dhiki" mara ,
na kila mtu anatumia mafundisho yaitwayo
"Unyakuo kabla ya dhiki," basi angalau mmoja
wa hiyo mistari au vifungu au sura
zingetufundisha kitu kuhusu unyakuo kutokea
kabla ya dhiki? Hata mmoja wa hiyo mistari
hausemi chochote kuhusu kuwepo kwa unyakuo
kabla ya dhiki au kitu kifananacho nayo,
kwa hiyo watu wanaoshikilia unyakuo kabla ya dhiki inabidi
wategemee tafsiri lukuki, na inabidi
wakueleze maelezo marefu, na mara zote
maelezo yao ni magumu kuyaelewa. Nimebaini jambo
fulani kuhusu Biblia: Mungu anataka tuielewe
Biblia. Hatufanyii michezo ya kuigiza
ili kutuchanganya na kufanya mambo yawe magumu.
Anataka tuuelewe ukweli. Anatupenda.
Nimebaini mara nyingi
Biblia inapoleta jambo kwa mara ya kwanza,
hutufafanulia, na kutusaidia tulielewe.
Kwa namna hiyo, tunapoliona kwa mara ya pili, tutajua ni nini anakizungumzia.
Biblia inasema katika Mathayo :
lakini hana mizizi ndani yake,
bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au
udhia kwa ajili ya lile neno,
mara huchukizwa.
Mch. Anderson: Waonaje ufafanuzi wa "dhiki"?
Udhia. Anasema
"dhiki au udhia" inayokuja sababu ya Neno.
Kwa hiyo hawa watu wanapitia
dhiki kwa sababu ni watu wabaya? Hapana,
wanapitia dhiki kwa sababu
wamesimama katika neno la Mungu. Na kwa sababu
wamesimama katika Neno la Mungu,
kwa sababu wamepokea neno la Mungu
kwa furaha,watapitia udhia
au dhiki. Kama tuna mizizi imara
katika tuaminicho, pale dhiki na udhia
vijapo, tutastahimili. Mara ya kwanza uonapo neno
"dhiki" likitumiwa kwenye Biblia,
linaambatana na neno "udhia." Yaani,
mara ya kwanza neno "dhiki" linatumika
katika Agano Jipya, na ukilifuata kila mara
katika Agano Jipya
neno "dhiki" linapotumiwa, % ya mara hizo linazungumzia waamini kupitia
dhiki - watu waliookolewa wanapitia dhiki.
Mara nyingine mbili zilizobaki linatumiwa mahali ambapo
halizungumzii watu waliookolewa, halizungumzii
kuhusu unabii wa siku za mwisho.
Linazungumzia tu kuhusu watu wanaopitia dhiki
kiujumla. Wakristo katika nyakati zote kihistoria
wamepitia dhiki, na katika kizazi chetu hatutakuwa
na tofauti yoyote. Labda
itatokea wakati wa uhai wetu, labda haitatokea
lakini ikitokea katika uhai wetu,
tutaipitia kama waamini. Ama tutauawa
kwa ajili ya Kristo, au tukijaliwa
tutavuka katika kipindi hiki na kuufikia
unyakuo.
Mara ya tano neno "dhiki" linatumiwa kwenye Agano Jipya ni kwenye Yohana :.
Mch. Anderson: Anaongea na waamini.
Anaongea na wafuasi wake. Anasema,
(Yohana :) Hayo nimewaambieni mpate
kuwa na amani ndani yangu.
Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo;
mimi nimeushinda ulimwengu.
Mch. Anderson: Alisema mtakwepa dhiki?
Alisema kwamba
hamtapitia dhiki? Je, alisema,
"Sitaacha watu wangu wapitie dhiki!
Nawapenda sana!" Hapana! Kwani Mathayo
inasemaje pale dhiki inapotajwa mara ya kwanza?
Kwamba kama watu hawana mizizi imara
,na dhiki au udhia ukitokea
kwa sababu ya neno, hawatastahimili.
Angalia aliyoyasema Yesu katika sura hii kwamba
anatuonya kuhusu dhiki katika mstari wa kwanza:
(Yohana :) Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
Mch. Anderson: Anasema kwamba asipokuambia
kuhusu haya, kama asipokuonya
kuhusu udhia na dhiki vijavyo
na majaribu utakayopitia
katika maisha, pale yatakapokuja, yatakustukiza
. Utaudhiwa. Utasema, "Kwa nini
unahubiri hivi, Mchungaji Anderson?"
Ninahubiri mahubiri haya ili usije
ukaja kuudhika. Utasema, "Hebu kwanza, mahubiri
haya yanaudhi!" Hapana, haya ni mahubiri ya
kukuzuia usije ukaja kuudhika kwa vile Yesu
alivyosema kwamba kama utajua yatakayotukia,
hautadhika. Angalia mstari wa :
(Yohana :) Lakini nimewaambia hayo,
ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke
ya kuwa mimi naliwaambia.
Sikuwaambia hayo
tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
Mch. Anderson: Kwa hiyo anasema hapa kwamba
Wakati mambo haya yakitokea mtakumbuka kwamba
Niliwaambia, na nawaambia kitu kilekile
Yesu alichokisema. Wakati mambo haya
yanaanza kutokea - inaweza isiwe wakati wa uhai wetu;
inaweza ikawa ni miaka kuanzia sasa; labda itakuwa
miaka kadhaa kuanzia sasa; hatujui lini mwisho\utakuwa - lakini utakapotukia,
mtakumbuka kwamba niliwaambia. Muhimu zaidi ya hivyo,
kwa sababu sikuyatunga mambo haya, mtakumbuka kwamba Yesu aliwaambia.
Mch. Jimenez: Mara nyingine unapokutana na neno
"dhiki" ni katika Matendo ya Mitume :, na
(Matendo :) wakifanya imara roho za wanafunzi
na kuwaonya wakae katika ile Imani,
na ya kwamba imetupasa kuingia katika
ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
Mch. Jimenez: Inavutia kuona tamko kwamba
imetupasa kuingia katika
ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi"
Mstari ulio bayana kabisa katika Biblia kwamba
tutaingia katika ufalme wa Mungu\kwa kupitia dhiki,
na siyo kuingia katika ufalme wa Mungu kabla ya dhiki.
Mch. Anderson: Kwani alisema,"Mtu uliye hai, ni
furaha iliyoje kwamba tutakuwa tushaondoka kabla ya dhiki!"
Hapana, alisema,"Ni vema kuwaimarisha. Ni
vema kuwaimarisha kwenye baadhi ya mambo.
Ni vema ukawaimarisha kwa sababu
ni vema wajue kabisa lazima wapitie
dhiki ili kuingia katika ufalme wa Mungu."
Unyakuo kabla ya dhiki umetajwa popote mara hii ya ?
Sidhani.
Mch. Jimenez: Katika Wakorintho :,
Biblia inasema:
( Wakorintho :) Ninao ujasiri kwenu; naona fahari kuu juu yenu.
Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha kupita kiasi.
Mch. Anderson: Hakusema, "Nina furaha kupita kiasi
kwa vile sipitii dhiki.
Nina furaha kupita kiasi kwa vile tutanyakuliwa kabla ya
dhiki!" Hayo siyo asemayo.
Alisema, "Katika dhiki yetu yote nimejaa furaha kupita
kiasi." U wapi unyakuo kabla ya dhiki
katika andiko hilo? haupo.
Mch. Jimenez: Inanivutia kwamba
kadiri unavyotazama neno "dhiki" katika
maandiko kikamilifu, utaona mistari kwa mistari
waumini wakielezea walivyopitia
dhiki. Anasema, "katika dhiki yetu yote."
Siyo kitu ambacho waamini hawatapitia
Ni kitu amacho waamini
wameshakipitia maisha yao yote.
Vizazi kwa vizai, waamini
wamepitia katika dhiki.
Mch. Anderson: Kumbukeni, ndugu, Mungu
hakusudii kutuchanganya. Hajaribu
kutuvuruga. Binadamu amekuwa akiwavuruga!
Wahubiri wamekuwa wakiwavuruga!
Vipindi vya TV na sinema zimekuwa vikiwavuruga
(Left Behind, nk.)
Mungu hawavurugi.
Mch. Jimenez: Kama tukiiruhusu Biblia iwe
kamusi yetu, na tukiiachia Biblia
ifafanue maneno kwa ajili yetu, tutaona kwamba neno
"dhiki" siyo ghadhabu ya Mungu.
Ni udhia. Ni mateso. Ni
matatizo.
Mch. Anderson: Unaweza kudhani kwamba mtu
angekuonyesha moja wa hizo mara inapotajwa.
Nionyeshe mstari mmoja unaosema kwamba
tutakuwa tushaondoka kabla ya dhiki, au kwamba
tutanyakuliwa kabla ya dhiki, au kwamba
unyakuo utatokea kabla ya dhiki.
Lakini ninaweza kukuonyesha wapi Biblia inasema
bayana kwamba mara tu baada ya dhiki,
Yesu atarudi na mawingu, na parapanda
italia, na wateule watanyakuliwa
kuwa pamoja naye mawinguni. Ni rahisi hivyo.
Wale waaminio katika unyakuo-kabla-ya dhiki
wanategemea wanadamu katika
kufafanua tafsiri na mantiki zao, na
"Mh, kwa vile hatujui siku wala saa,
ina maana inaweza kutokea wakati wowote,
na kama inaweza kutokea wakati wowote, basi ni
lazuma iwe kabla ya dhiki kuu." Au watakuwa
na majedwali tata ili kukuelezea.
Lakini tu ukichukua Biblia na
kuyachukulia yale isemayo kama yalivyo -
soma kuanzia Mathayo - pale ufikapo Mathayo
, utaikuta, bayana kama mchana: BAADA YA
DHIKI Yesu anakuja mawinguni.
Mch. Anderson: Dk. Kent Hovind ni mwinjilisti
mashuhuri kweli aliyeamini na kuhubiri
unyakuo kabla ya dhiki kwa miaka . Sasa yeye
yuko kifungoni, na tangu awe
gerezani, amekuwa akijisomea Biblia yake, na
kubaini kwamba unyakuo kabla ya dhiki haumo
kwenye maandiko, na nataka kumsikia
ili kubaini ni nini kilimfanya
abadilike. Nini kilimfanya agundue kwamba ni
BAADA YA DHIKI?
Dk. Kent Hovind: Jina langu ni Kent Hovind.
Nilikuwa mwalimu wa sayansi kwa miaka vidato vya juu
na kisha nikawa mwinjilisti kwa miaka
nikifundisha uumbaji na mageuko. Na
Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu mtazamo wangu
wa nyakati za mwisho na vipi unaendana na maandiko,
na nikashawishika, miaka mitatu hivi iliyopita,
kwamba yale niliyofundishwa miaka yote ya maisha yangu,
si ya kweli. Ilinibidi kubadilika, kwa masikitiko ya
ndugu wengi wasiokubali kubadilika,
na kuhamia kwenye unyakuo-baada-ya-dhiki,
kabla-ya-hukumu. Biblia inasema siku za mwisho
watu wadharauo watapuuza uumbaji, na
mafuriko, na hukumu inayokuja. Kwa kweli, nilitumia
miaka kufundisha duniani kote kuhusu
uumbaji na mafuriko, lakini
niliacha ile sehemu ya hukumu inayokuja kwa vile
sikuielewa mimi mwenyewe. Katika Mathayo
, mafundisho ya Yesu yanatupatia kile
wanafunzi wake walimuuliza kwa wazi: nini
itakuwa ishara ya kurudi kwako? Na ni lini itatukia?
Maelezo hayohayo yanarudiwa katika Marko
na katika Luka , hivyo nilinakili kurasa toka
katika Biblia zenye maelezo hayo toka vitabu vyote vitatu na
kuvipanga kimoja pembeni ya kingine.
Mara ukishabaini
maelezo yote, inakuwa wazi kabisa
kwamba unyakuo kabla ya dhiki hayakuwa mafundisho ya kweli.
Mch. Anderson: Kwa nini unafikiri kwamba watu wengi/N bado wanaamini katika unyakuo -kabla ya dhiki?
Kwa nini mafundisho haya ni mashuhuri sana?
Dk. Kent Hovind: Kwa sababu yanatatua tatizo
linaloonewa aibu. Wakristo hawakuweza kujibu
maswali kuhusi dinosori. Wanasemaje?
Kwa hiyo, walibuni mafundisho ya "gap theory" na
watu wakawaamini. Nadhani wazo la unyakuo bila dhiki
unaangukia katika fungu hilohilo ambalo watu
wana masikio yanayowawasha. Haya ndiyo
wanayotaka kuyasikia.
Mch. Anderson: Sawa.
Mch. Kent Hovind: Wanataka kusikia, "Hee!
Sitalazimika kupitia taabu." Lakini Yesu
alisema kinakuja kipindi cha dhiki
ambacho hakijawaki kuwepo tokea ulimwengu kuwako. Yaani,
unadhani mateso ya kule Hispania yalikuwa mabaya?
Au Manazi walivyowaua Wayahudi
yalikuwa mabaya? Au vile Warumi walivyotesa Wakristo?
Itakuwa ni mbaya kuliko hayo yote yakichanganywa pamoja!
Mch. Anderson: Mh. Inashangaza.
Dk. Kent Hovind: Kwa hiyo, dunia inaanza kwa
Kaini kumuua Habili - waovu kuwa wema.
Mch. Anderson: Ni kweli.
Dk. Kent Hovind: Imekuwa hivyo mara zote
ukitazama historia. Na Yesu alituambia
watakapokuwa wakiwaua au kuwatesa, furahini,
kwa sababu thawabu yenu ni kubwa katika ufalme wa mbinguni.
Mch. Anderson: Kama hakika tukichukulia Biblia
isemavyo kuhusu nini maana ya "dhiki" (siyo
maana iliyochakachuliwa) - kama
tukichukulia maana halisi ya kibiblia ya
"dhiki," huwezi kusema tunapitia dhiki
hivi sasa?
Mch. Kent Hovind: Ah, ndiyo. "Dhiki" ndicho
dunia inatutendea, na tayari
imeshatokea ma maelfu ya miaka. Yesu alisema,
"Duniani mna dhiki: lakini
jipeni moyo: mimi nimeushinda ulimwengu."
Wakristo wategemee dhiki, na
tutapata thawabu tukiipita kwa uvumilivu.
Mch. Anderson: Sasa, kwa vile somo hili ni kuhusu
"Msimamo Mkali wa Kidini," linaweza
kuangukia katika fungu la mawazo ya watu,
kudhani kwamba kutakuwa na mwisho
wa dunia - kwamba kutakuwa na kurudi kwa Yesu
Kristo kama kulivyoandikwa. Ndiyo
maana nilitaka kukueleza kwa kifupi
Nikupe to mwongozo mfupi
wa kile kitakachokuja kutokea kwa mujibu wa
Biblia, na ni vipi yote yatatokea.
Mch. Anderson: Nadhani ufunguo wa kukielewa
kitabu cha Ufunuo ni kuelewa
kilivyogawanywa. Mungu alitupa kitabu cha Ufunuo
kiwe hivyo - ufunuo - kitufunulie
vitu hivi, siyo kuvificha. Siyo
kitabu cha Kujificha. Ni kitabu
cha Ufunuo, na Mungu anataka kieleweke
kwa urahisi. Ndiyo maana alitupatia
kwa muundo ambao ni rahisi kuuelewa. Unapoanza kusoma sura ya kwanza,
unaona nyakati za Kristo au karibu nao kwa vile
Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo, na Yohana
alikuwa akiteswa kwa kuhubiri Injili,
kwa hiyo tunaongelea pungufu ya karne
baada ya Yesu kuja duniani hapa. Kisha
anapokea maono ambayo anamuona Bwana
Yesu Kristo akimtokea. Kisha katika sura za -
Yesu Kristo anampa ujumbe
kwa makanisa saba ya Asia, na ni wazi
makanisa hayo yalikuwepo katika karne ya
kwanza., wakati huo. Kisha katika sura za
- tunakuta maono ya Mbinguni ambapo
anaelezea yanayotukia Mbinguni. Kisha katika
sura ya tunaona matukio ya
wakati wa dhiki kuu. Sura ya ndipo mkutano
mkuu unaotokea Mbinguni - wazi ndio
unyakuo - mataifa yote na watu wote\wanawakilishwa hapo. Kisha katika sura ya
Mungu anamimina ghadhabu yake juu ya dunia hii.
Kisha sura ya ni sura maalumu
inayozungumzia mambo kadhaa kabla ya
baragumu ya kupigwa. Kisha katika sura ya
baragumu ya inapigwa. Yote haya ni kusema hivi:
ukiangalia kitabu cha Ufunuo,
sura za kwanza zinafuata mtiririko
ambao unaleta maana kamili kabisa. Unaanzia
wakati wa Kristo, mpaka karne ileile aliyokuwepo
Kristo. Kisha unaenda kwenye matukio ya
baadaye: dhiki kuu, na kisha unyakuo, na kisha
Mungu akimimina ghadhabu yake. Kisha pale
baragumu ya saba ikipigwa katika sura ya , ambapo pana utimiifu, asemapo, "Ufalme wa
dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki
hata milele na milele. Lakini kinachovutia
ni kwamba uendapo mwisho wa sura
ya , unakutana na utimilifu huo mwishoni. Sawa,
unapoingia sura ya , na hapo
pana badiliko kubwa katika kitabu cha Ufunuo
kwa sababu angalia mstari wa wa sura ya . Unasema:
(Ufunuo :) Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa
jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
(Ufunuo:) Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu,
alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
(Ufunuo :) Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha
katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa,
ili azaapo, amle mtoto wake.
Mch. Anderson: Sasa angalia kwa makini
mstari wa .
(Ufunuo :) Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa
fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
Mch. Anderson: Ni wazi kwamba mtoto huyo ni
Yesu Kristo kwa vile katika Agano la Kale
na Agano Jipya, Biblia inamtaja Yesu Kristo
akitawala dunia kwa fimbo ya
chuma, na inazungumzia utawala wake ujao wa
miaka elfu moja. Hivyo
njia nyepesi kabisa ninayoweza kukusaidia kukielewa
kitabu cha Ufunuo ni kukwambia kigawe
mara mbili pale katika sura ya . Sura ya - nusu
ya kwanza, na - nusu ya pili. Kisha kama
ukiziweka nusu hizo moja pembeni ya nyingine,
utayaona matukio yaleyale kwa mitazamo miwili tofauti:
Mch. Anderson: Kwa nini Mungu afanye hivyo?
Kwa nini Mungu asimulie kitu hichohicho mara mbili katika
kitabu cha Ufunuo? Ni kwa nini alituambia
Injili mara nne katika Mathayo,
Marko, Luka, na Yohana? Kwa nini alitupa kitabu cha
& Samweli na & Wafalme, lakini
pia akatupa & Nyakati kutupa
fursa ya mtazamo, mwonekano, mingine na
tujifunze mengi kwa kulinganisha vitabu
vyaWafalme na vitabu vya Mambo ya Nyakati,
au kilinganisha Mathayo na Marko, na Marko na
Luka, na Luka na Yohana, na hivi vimetupa
mitazamo tofauti. Hivyo kwa njia hiyohiyo
tutaweza kukielewa kitabu cha Ufunuo.
Hivyo itakuwezesha kuelewa kitabu cha Ufunuo
pale unapoelewa mfululizo wa matukio.
Wapo watu wanaodhani kitabu cha Ufunuo hakina mtiririko wowote, lakini neno
"baada ya haya" au msemo "baada ya mambo haya"
unatokea mara katika kitabu cha Ufunuo.
Kama tukiona tena na tena "baada ya haya"
na"baada ya mambo haya,"
Mungu anatupa mpangilio wa matukio.
Mch. Jimenez: Inashangaza kujaribu
kutafsiri Biblia au kusoma Biblia
ili kukabili upinzani kwamba japo Biblia inasema
"baada ya haya," watu wanasema "hayako kwa mpangilio
wa muda. Inashangaza kabisa." Mahali pote kwenye
Biblia, hivyo ndivyo unavyosoma maandiko.
Mfano mzuri: katika Yohana:, inasema:
(Yohana :) Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru,
ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
Mch. Jimenez: Kisha katika mstari wa anasema,
"Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake
walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi;" na itakuwa ni
wehu mimi kusimama hapa na kusema,"Hapana,
mstari wa hasa ulitukia kabla ya mstari wa
," wakati mstari wa unasema "baada ya hayo."
Tungeangalia na kusema, Haswa,
ndivyo ilivyoandikwa, na hivyo ndivyo
ina maana. Kisha tufikapo katika kitabu cha Ufunuo,
na kama nilivyosema, mara unasoma "baada
ya hayo" au "baada ya hili," lakini bado wapo watu
wanaosema, "Hamna, hayako kwa mpangilio wa wakati.
Haileti maana." Ni namna ya kijuha
kusoma Biblia.
Mch. Anderson: Kwa hiyo, ukishafahamu kwamba
ni kwa mpangilio, lakini unaoanza tena
katika sura ya , itakusaidia kuelewa.
Nataka kupitia sura kadhaa
hapa kukuonyesha mpangilio wa matukio ya
siku za mwisho. Haya yanaweza kutokea miaka toka
sasa. Tunaweza kuwa tushaondoka, lakini nadhani
uwezekano mkubwa yatatokea
si mbali sana. Kwa kweli, nadhani nitashangaa iwapo
mambo haya hayatoteka walau katika
uhai wangu kama nitajaliwa kuishi miaka ya kawaida.
Na sasa nina miaka , na kwa kasi ya
vile mambo yanaenda sasa, nitashangaa
iwapo haya hayatatokea ndani ya miaka ijayo.
Nitakapoanza kuufikia ujumbe huu leo,
natumai utaelewa zaidi kwa nini
ninasema hayo. Hiki ndicho kinachoanza
dhiki. Biblia inasema kwamba Ibilisi,
au Shetani, atatupwa kutoka Mbinguni. Najua
utasema, "Ngoja kwanza, Mch. Anderson,
hayo kwani hayajatokea tayari?" Lakini jibu ni
hapana. Watu wanadhani kwamba Ibilisi yuko Kuzimu
hivi sasa, lakini kiukweli, Ibilisi hajawahi kuwemo
Jehananum kwa vile Biblia inaweka
wazi kabisa kwamba Ibilisi yuko Duniani humu
akizungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta watu
wa kuwameza. Ibilisi na mapepo yake
wapo duniani humu ukisoma Biblia.
Huenda na kurudi baina ya Duniani na Mbinguni,
na huzungumza na Mungu. Ukisoma kitabu
cha Ayubu, Ibilisi huja na kusimama mbele za
Mungu na kuwa na mazungumzo na Mungu Mbinguni
kuhusu mtumishi wa Mungu Ayubu. Kwa hiyo Ibilisi
hivi huenda na kurudi. Hivyo, Biblia inazungumzia
kuhusu siku moja ambayo Shetani atatupwa
kutoka Mbinguni:
(Ufunuo :) Kulikuwa na vita mbinguni;
Mikaeli na malaika zake wakapigana na
yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
(Ufunuo :) nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
(Ufunuo :) Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi
na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi,
na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
(Ufunuo :) Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na
nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa
ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
(Ufunuo :) Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno
la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
(Ufunuo :) Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi
na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi,
akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Mch. Anderson: Tunaona nini hapa?
Pana vita Mbinguni, na Biblia inafundisha
kwamba Ibilisi atashindwa vita hiyo. Atapoteza
vita hiyo Mbinguni, na kwa sababu atashindwa
vita, yeye na malaika zake, ambao hapa tunaona
kwamba ni theluthi ya malaika, wao
watatupwa duniani. Kimsingi, Shetani kutupwa
kutoka Mbinguni, naye akijua
kwamba muda wake ni mchache, naye atatoka
ili kuwatesa waamini na kuwatesa
watakatifu na kujaribu kuwaangamiza. Angalia
sura ya . Hapa ndipo ile vita inaanza.
Katika Ufunuo :, atatoka kufanya vita.
Atafanyaje? Ibilisi atafanyaje
vita dhidi ya waamini?
Mch. Anderson: Kitu kingine tutakachokiona
kilichotabiriwa kutokea ni kile kiitwacho
dhiki kuu. Dhiki kuu ni kipindi ambacho
kutakuwa na mambo mengi yatokeayo
katika dunia hii ambayo ni ya maangamizi.
Kutakuwa na njaa. Kutakuwa na tauni.
Kutakuwa na vita - kiwango cha kutisha cha vita.
Watu wengi watakufa kwa njaa
na magonjwa. Mambo mengi mabaya
yatatokea. Yaani, kati ya
hivi vita na maafa yatakayotokea wakati wa dhiki
(siyo ya miujiza
siyo Mungu akinyesha mvua ya moto na kiberiti,
lakini majanga ya asili, vita, baa la njaa,
yaliyosababishwa na binadamu) patakuwa na mtu atakayeibuka na kuwa dikteta
wa dunia nzima ajulikanaye kama "mpinga kristo"
Haya si hadithi za kutunga. Haya kweli
yatatokea, na hakika, tunaweza kuona tayari
dalili kwamba yameanza kutokea.
Biblia inatuambia kwamba siku moja patakuwa na
serikali moja ya dunia. kwa sasa tunazo
serikali nyingi tofauti. Tuna Marekani, tuna Urusi
,tuna China, hizo
zote ni nchi huru tofauti (Umeshasikia neno hili
"huru" - hayo yote
ni mataifa tofauti. Kwa hiyo, siku moja, Biblia inasema
nchi hizo zote zitakuwa
zimeunganishwa na kutengeneza serikali moja ya dunia.
Zikishatengeneza hiyo serikali moja ya
dunia, watakabidhi madaraka yote kwa mtu
mmoja, atakayekuwa mkuu wa serikali hiyo,
na mtu huyo atajulikana kama "mpingakristo."
Nani alishawahi kusikia kuhusu mpingakristo?
Kila mtu ashawahi kusikia jina hilo. "Mpingakristo"
ni neno litokanalo na Biblia. Utasikia mara kwa mara
Biblia ikiongelea kuhusu "mnyama" au "mnyama toka
baharini," au "mnyama mwenye sura saba
na pembe kumi," au "mtu mwenye dhambi," au
"mwana wa uharibifu," lakini pia Biblia inatumia
neno "mpingakristo." Napenda kutumia neno
"mpingakristo:" linaeleweka kirahisi
na ni la kibiblia. napenda kukuonyesha wapi
Biblia inalitaja jina
"mpingakristo" kwa vile Biblia inatuambia kwamba
atakuja mtu nyakati fulani ambaye ataitwa
mpingakristo. Kabla Yesu Kristo hajarudi tena
patakuwapo na tapeli, Kristo bandia.
Unanielewa sawasawa? Mpingakristo ni mtu
atakajidai kuwa ndiye kurudi mara ya pili kwa
Kristo, wanafundishwa kutarajia
Yesu kurudi wakati wowote, itakuwa sawia
kwa sababu, unajua nani atakeyejitokeza-
mpingakristo. Kwa nini Biblia inamuita 'mpingakristo'?
Kwa sababu pana mtu anakuja akiitwa 'mpingakristo.'
(siyo wapingakristo) ambaye atasema kwamba yeye ni Yesu Kristo.
Pale mpingakristo akiibuka wakati wa dhiki kuu
na kusema, "Mimi ni Yesu Kristo," watamkubali kama
vile yeye ni masihi. Watu wengi
watafundisha, "Unajua, Yesu Kristo arudipo mawinguni,
Wayahudi hatimaye watabaini kwamba
alikuwa ndiye masihi, na kwamba watampokea.
Hapana, watampokea mpingakristo!
Ndicho Biblia inachokisema. Yesu alisema:
(Yohana :) Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija
kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
Mch. Anderson:Nadhani mpango wa Shetani kuleta
mafundisho ya unyakuo kabla ya dhiki ni kuandaa
mawazo ya kila mtu kwamba "Yesu Kristo
atakuja dakika yoyote." Tunamtarajia
Yesu Kristo muda wowote! Anaweza kuja leo!
Anakuja leo!" lakini kikweli hasa
mtu anayekuja ni mpingakristo. Na ajapo
mpingakristo, atakuwa ndiye
mkuu wa serikali moja ya dunia na dini moja
ya dunia ambapo atadai kuwa yeye ndiye masihi.
Inasema katika mstari wa wa Yohana :
( Yohana :) Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo
yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
Mch. Anderson: Huo mtajo wa kwanza ni uingi au umoja?
Kwa hiyo wameshasikia kwamba mpingakristo
(umoja) atakuja. Hivyo pana mpingakristo fulani ajaye
,au hakuna? Lakini hakuna wapingakristo
wengi hata sasa? Ndivyo mstari huo unavyosema
Ni nani hawa wapingakristo?
( Yohana :) Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo,
yeye amkanaye Baba na Mwana.
Mch. Anderson: Ili kuamini kwamba Yesu siye
Kristo, inabidi kuamini
kwamba pana Kristo, lakini siyo Yesu.
Neno "Kristo" maana yake "Masihi."
Biblia inasema katika Yohana :," Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake,
Kristo). Kwa hiyo Biblia inatafsiri neno "Kristo"
kuwa ni "Masihi". Haya mawili ni sawa kabisa.
Acha nikuulize: Unafikiria dini ipi iliyoko ambayo
inasema kwamba pana
masihi atakayekuja, lakini masihi huyo si Yesu
-Yesu hakuwa huyo masihi. Dini ya Kiyahudi inafundisha
kwamba pana masihi, sawa, lakini hatakuwa
Yesu. Bado wanamsubiri
masihi. Wanasema kwamba yesu hakuwa ndiye
masihi, na kwamba bado wanamsubiri
masihi. Biblia inasema kwamba watampokea
mpingakristo kama masihi wao. Wakristo wa
Kiinjili wanaamini kwamba Yesu anaweza kuja
muda wowote, wale wasiookolewa,
wale wasioamini kweli,
wengi wao watadanganywa na kudhani,"Huku
ndiko kule kurudi mara ya pili kwa Yesu Kristo!"
Waislamu leo hii bado wanamngojea nabii mkuu
na masihi atakayekuja ambaye hakika ni mkuu
kuliko Mohamed. Rais Ahmadinejad,
Rais wa Iran - nani ashamsikia? Rais Ahmadinejad
alihutubia
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka mmoja au
miwili iliyopita,
na alipohutubu, alitoa ufafanuzi mfupi wa Uislamu.
Mahmoud Ahmadinejad: Kimsingi ujumbe mkuu wa
manabii ni uleule mmoja. Kila mjumbe
alimthibitisha mjumbe aliyemtangulia na
kutanguliza habari njema za nabii atakefuatia
ambaye atatoa habari kamili za dini
kwa kadiri ya uwezo wake
kwa wakati huo. Mwelekeo huu umeendelea mpaka
kwa mjumbe wa Mungu aliyeeleza kikamilifu
dini ikusanyayo wote. Nimrod alimpinga
nabii Ibrahimu Farao alimpinga Musa
na choyo kilimpinga nabii Yesu Kristo
na nabii Mohamed
amani iwe kwao manabii wetu wote hao.
Mch. Anderson: Na akasema kwamba Uislamu unaamini
kwamba Ibrahimu alikuwa nabii mkuu, Musa
alikuwa nabii mkuu, na kisha alikuwepo Yesu,
na tena akawepo Mohamed - na Muislamu huyu
anatikisa kichwa chake kwa hiyo nitakuwa napatia!
Na kimsingi alichosema Ahmadinejad
ni kwamba kila mmoja wa watu hao alileta hadharani
ukweli mwingi zaidi kuliko aliyemtangulia kwa kuwa
binadamu walikuwa tayari zaidi kupokea. Walileta nuru
kubwa zaidi, maelezo na ukweli zaidi. Alisema kwamba
baadaye nabii mwingine ataibuka ambaye atakuwa
mkuu zaidi hata kuliko Mohamed na
ataleta kiwangu kikubwa zaidi cha nuru. Hivyo Uislamu
unatarajia masihi ajaye.
Wanamtarajia Imamu Mahdi.
Mahmoud Ahmadinejad: Ee Mungu, harakisha kuja
kwa Imam al Mahdi na umpe afya njema
na ushindi, na utufanye sote wafuasi wake, na
wale watakoshuhudia alivyo mwenye haki.
Mch. Anderson: Wabudha wanasubiria kuja kwa
Budha wa Tano. Wote hao
waliko Tibeti wanamfuata Dalai Lama: wanaamini
kwamba Dalai Lama huzaliwa upya
ndani ya mtu mwingine - ile roho ya Dalai Lama
Wataaminii kwamba mpingakristo
ni mtokeo mpya wa Dalai Lama. Waislamu
watamwona kama ndiye Imamu Mahdi.
Wakristo watamwona kama Kristo aliyerudi/N mara ya pili. Wayahudi watamwona ndiye
masihi. Dini zote hizi kuu zijamuunga mkono
na watu watasema,
"Furaha iliyoje kwamba hatimaye tunaungana!
Tunaweka mbali tofauti zetu, na huyu
mtu ni wa ajabu!" na watamwabudu
mtu huyu. Huyu tapeli, huyu mpingakristo,
atakuja. Serikali ya dunia itamweka madarakani
na kumpa mamlaka yote,
na watamtangaza kwamba ndiye Mungu.
Watamtangaza kwamba ndiye kurudi kwa pili
kwa Kristo. Atauawa. Biblia inasema atapokea jeraha la mauti
kichwani mwake, jeraha lile litapona,
na atafufuka. Kisha
atajitokeza kudai yeye ndiye kurudi kwa pili kwa
Yesu Kristo. Atatangazwa kuwa
ni Mungu katika mwili, na mataifa yote ya dunia
watu wote wa dunia
watamwabudu mtu huyu. Kimsingi kila dini
itamkubali kwamba ndiye masihi, lakini
Biblia inasema kwamba wale waliookolewa
hawatadanganyika. Waliobaki wote
watamwabudu na kumwamini kwa sababu
atafanya miujiza, na Biblia inasema,
atafanya ishara zote hizi, na maajabu
na ataleta hii
serikali ya dunia. Wakati mwingine unajaribu
kuwaonya watu kuhusu serikali moja ya dunia.
Unajaribu kuwatahadharisha kuhusu mielekeo
ambayo tunaiona ikitokea kuelekea jamii isiyotumia
fedha taslimu. Tunawaona Wakristo wengi ambao
-unaongea na Wakristo kuhusu serikali moja ya
dunia, au unaongea nao kuhusu jamii isiyotumia
fedha taslimu na mambo haya yote
yanayowekwa na serikali katili,
na watakupachika jina la "mnadharia za kijuha."
Nina hakika ushaitwa mnadharia za kijuha
katika miaka yote hii.
Dk. Kent Hovind: Ndiyo, mara nyingi tu.
Mch. Anderson: Lakini mtu yeyote anayeamini kweli
Biblia anaweza kukanusha kwamba
patakuja kuwa na serikali moja ya dunia nyakati
fulani?
Dk. Kent Hovind: Sidhani kama unaweza kusoma Biblia
bila kuona ukweli kwamba
ni mpango wa siku zote wa Shetani wa kutawala dunia
kama karikenye, na anataka serikali
moja ya dunia. Anataka awe ndiye Mungu.
Mch. Anderson: Wakati mtu huyu akitawala dunia
nzima, atamuamuru kila mtu
apokee kile kiitwacho "alama ya mnyama."
Nani ashasikia kuhusu alama ya mnyama?
Biblia inasema kwamba alamya ya mnyama
itakuwa kitu fulani mkono wa kuume au katika
paji la uso, na hakuna mtu atakayeweza kuuza au kununua pasipokuwa na alama hii.
Watu wangapi waliosoma haya karne kadhaa zilizopita
na kusema,"Itawezekanaje? Atawezaje
kuwazuia watu kuuza au kununua
mpaka wawe na chapa yake?Hauwezi tu kutoa
pesa taslimu?" Angalia teknolojia ilipofikia.
Pesa hizi nilizozishika mkononi,
hii fedha ya noti, ni kipande cha karatasi.
Hakina thamani yoyote. Hakina thamani yoyote ya kwake yenyewe.
Unapoanza kuona jamii isiyotumia fedha taslimu ikijitokeza
tunazidi kwenda mbali zaidi kuacha kutumia fedha taslimu
Mtu kwenye TV: Patakuwa na muda ambapo fedha
taslimu itapitwa na wakati.
Mtangazaji: Kwa hiyo pesa za karatasi ni masalia
ya mambo ya kale?
Mtu kwenye TV: % ya miamala yote Marekani
au zaidi sasa hufanyika pasipo kuhusisha
fedha taslimu za karatasi au sarafu.
Mama Mtangazaji: Ushawahi kujiuliza iwapo siku moja
fedha taslimu zitaacha kuwepo?
Ni ukweli kwamba wengine wanasema tukubali tu
kwamba fedha taslimu ni kero tu.
Afisa Mwafrika: Kanuni ni kwamba ni lazima
tutoke kwenye uchumi wa fedha taslimu
kuelekea uchumi usiotegemea fedha taslimu. Hii
inahusisha mabenki. Inahusisha makampuni ya mawasiliano.
Inahusisha wenye ATM na mashine kutolea risiti.
inahusisha kubadilisha utamaduni.
Mtangazaji: Unazipa pesa jina gani siku hizi?
Je, ni kiasi fulani cha sarafu na manoti?
Au kadi ndizo zinazotamba? Na aina zetu fulani
za hela zinafikia ukomo wa matumizi,
Dk. Kent Hovind: Chukua kwa mfano kila duka mjini
kwenu likisema,"Hatukubali tena pesa taslimu,"
na mfano wakisema, "hatukubali pia matumizi ya
hundi au kadi za benki kwa vile pana
wizi mwingi -- kadi nyingi zilizoibiwa
na hundi nyingi zisizo na hela kweli.
Lazima tukubali. Pesa za noti hazina thamani yoyote ya kweli.
Ni kipande tu cha karatasi. Ingeweza hata kuwa ni
pesa za kuchezea mchezo wa Monopoly. Siyo dhahabu. siyo
fedha. Haina thamani yoyote ya ukweli. Kwa hiyo,
kwanza walituzoesha kutumia vipande vya
karatasi ambavyo havina thamani yoyote. Leoo hii naweza
kubadilishana kipande hicho cha karatasi na huduma na bidhaa
lakini mtu mwingine akisema kesho, "Hiyo hela haina
thamani yoyote," basi haitakuwa
na thamani yoyote. Unakumbuka Majimbo ya Kusini
mwaMarekani? Unakumbuka vile Wakonfedereti hao
walikuwa na pesa yao? Watu waliweka pesa za
Wakonfedereti kwenye magodoro. Unajua nini, hazikuwa
na thamani yoyote tena. Ndiyo, wanaweza kukutendea
hivyo na wewe, na kusema,"Pesa zako za noti
hazina maana tena. Kila kitu kitaangaliwa kwenye
akaunti yako tu. Vyote vimeunganishwa na Facebook na Youtube
na gmail yako, na ni vema kwa vile hakuna
tena ubadhirifu. Huhitaji
kuhofia kuacha waleti yako nyumbani.
Huwezi kuhofia kuhusu kadi yako ya benki
itaibiwa. Ni jamii isiyotumia kabisa pesa taslimu.
Tunaweza kudhibiti madawa kwa vile
hakutakuwa na miamala ya pesa taslimu.
Ni njia pia ya kuzuia uhalifu.
Mama Mtangazaji: Ni kama hadithi za kufikirika kuhusu
zinazotaka kuwa kweli katika maduka kwa kisingizio
cha kuongeza ufanisi. Utaweza kununua chochote
kuanzia mkate hadi vinywaji kama ukikubali
kulipatia duka kitambulisho chako.
Mtu wa ACLU: Inanitisha kweli.
Mama Mtangazaji: Mara wakishakagua unavyotaka kununua
nini kinafuata? Unaweka kidole cha shahada
kwenye kifaa kinachosoma, na hapo utakuwa umelipia
ndani ya sekunde tatu kwa kugusa tu
na kidole chako. Inaitwa Baiometria: Njia
otomatiki ya kukutambua
kulingana na maumbile yako ya tofauti na wengine kibailojia.
Mtu wa ACLU: Usikubali mambo haya kwa sababu tu ya
urahisi.
Mfanyakazi wa zamani wa QT: Unajua, hivi leo
alama za vidole, kesho ni kipandikizi.
Labda hiyo ndiyo inaashiria alama ya mnyama.
Mama kwenye TV: Huyu jamaa aliacha kazi yake ya utawala
katika Quik Trip pale maduka hayo
yalipomwambia lazima atumie alama za vidole
katika kuripoti kazini na kuripoti kuondoka.
Mwajiriwa wa zamani wa QT: Na ingawa hivi sasa
ni mpango wa hiari, nani ajuaye kuhusu kesho.
Mama kwenye TV: Wataalamu wanasema kwamba baiometria
zinakaribia
kuvamia nyanja zote za kiuchumi na maisha yetu ya kila siku.
Mama kwenye TV: Unaweka kidole chako kwenye kifaa chao,
na jina langu linatokea, na anapata taarifa zangu zote.
Mtangazaji: Ni haraka hivyo?
Mama kwenye TV: Ni haraka sana.
Unaipenda? Utaienda.
Mama Mtangazaji: Watu duniani kote tayari wanatumia
baiometria. Serikali ya Marekani, mashirika ya ndege,
vituo vya mafuta - hata Walt Disney World wanatumia
teknolojia inayoweza kusoma mishipa ya damu
badala ya kuchukua vitambulisho vipya kila siku kwa wanaoitembelea.
Mch. Anderson: Hii serikali moja ya dunia itakuwa na
nguvu sana kiasi kwamba itaweza
kuamrisha kwamba hakuna mtu duniani hapa ambaye
ataweza kununua na kuuzia bila kuwa na
alama ya mnyama. Najua inasisimua kuona kwamba
Biblia inatafsiri wazi kabisa kwamba
alama ya mnyama - hi alama itakuwa lazima kuwekwa
kabla ya kuuza au kununua -
itakuwa NDANI ya mkono wa kulia au NDANI ya
mapaji ya uso. Hii inaweza kuwa aina flani ya kipandikizi
ambacho ili ununue au kuuza, unahitajika
kuskani hiki kipandikizi. Kitu
kitakachokuja kutokea siku moja ni kwamba watasema,
"Hizi pesa za noti - noti ya dola mia
mfukoni mwako - haina thamani tena. Lazima uskani
kulipia. Kila kitu ni kielektroniki. Ukienda
dukani, na kukusanya unavyotaka kununua, kisha
*Mlio wa tindo*. Kama huna
mkono, hakuna shida, tunaweza kukiweka kipandikizi
kichwani pako kwa vile kila mtu ana kichwa!
Utatoa pia *mlio wa tindo* wakati wa kulipia. Kila
pesa itakuwapo kieletroniki, na
tayari mwelekeo ni huo. Simu za mkononi tayari
zimeanza kuwa na skana. Tuseme,
pana mauzo ya bidhaa na huduma baina ya watu wawili.
Sawa, itakuwa dola ..
Nionyeshe tu mkono wako wa kulia, nami
nitauskani kwa simu yangu ya kisasa. *Biiip*
Sawa, sasa nimechukua fedha toka kwenye akaunti yake.
Na, hivi punde tu umemfundisha mwanangu kupiga kinanda.
Acha nikulipe. *biiip* Hebu itafakari sana:
Simu ya kisasa inaweza kutumika kuskani alama ya
mnyama, na huwezi kununua au kuuza bila hiyo.
Mama Mtangazaji: Katika habari za afya leo hii, kipandikizi
chenye ukubwa wa mchele kinaweza kuokoa maisha yako.
Mtangazaji: Mwaka ni . Umekimbizwa hospitali
haujitambui bila kitambulisho wala vyeti
vya hospitali, lakini shauri ya kipandikizi chini ya
ngozi yako, taarifa zote ziko humo. Hadithi za kufikirika miaka
iliyopita, lakini baiometria ni hali halisi leo hii.
Profesa: Nadhani inawezekana kabisa kuacha kutumia
waleti na funguo kwa
kuhamia kwenye teknolojia ya baiometria kama ndicho
watu wanakitaka ndani ya miaka ijayo.
Mtangazaji: Changamoto ni kulinda taarifa zetu binafsi
katika ulimwengu huu mpya.
Mtangazaji: Teknolojia mpya ya vipandikizi sasa
inawezesha wafanyakazi wa vitengo vya dharura hospitalini
kubaini historia yako ya matibabu kwa
kubofya tu kwenye kompyuta.
Daktari wa Harvard: Matabibu wengi wa dharura
wanalazimika kufanya upasuaji bila kufahamu mengi. Tunalazimika
kuchukua maamuzi ya kidaktari bila kujua dawa zipi
ulizotumia au una mizio ipi.
Mtangazaji: Dokta wa Havard anasema kwamba hiki kifaa cha
Radio Frequency Identification Chip kitatatua
tatizo hilo. Alikipandikiza katika mkono wake wa kuume.
Skana inaweza kusoma utambulisho
wake. Tarakimu hizo hatimaye huingizwa kwenye
wavuti salama ambako taarifa zake za matibabu
hutunzwa. Mfanyakazi wa hospitali anasema kwamba
kipandiki kinaweza kuwasaidia watu wa kitengo cha matibabu ya dharura.
Mfanyakazi wa Dharura: Moja ya mambo makubwa
unayoweza kukutana nayo kwa majeruhi wanapowasili
na wasiweze kukupa taarifa yao yoyote
na au historia yao ya matibabu.
Mtangazaji: Dokta wa Havard anasema kwamba
manufaa ni wazi.
Dokta wa Havard: Mimi ni mpanda majabali, na
naamini kwamba nikidondoka, na
ukanikuta sina fahamu, faida ya kuweza kuniskani
na kubaini mimi ni nani inapiku
msimamo wangu kuhusu haki ya taarifa zangu binafsi.
Mtangazaji: Kipandikizi hufichwa ndani ya kioo
kisichovunjika na kina ukubwa karibu sawa na punje ya
mchele. Upandikizaji hufanywa chini ya nusu-kaputi
na kwa ujumla hauna maumivu.
Dokta wa Havard: Ni kama kuweka korochea
chini ya ngozi yako.
Mtangazaji: Lakini kwa hili, anasema kwamba
kuweka kitu chini ya ngozi yako ni vema
Mtangazaji Mwanaume: Huanza kama hivi: huyu ni
paka, miaka mitano baadaye, tunagundua kumbe
amerudi. Mwingine atasema, Unajua kama inafaa
kwa paka, ninao
baba na mama nyumbani na baba huwa anapotea
mara nyingine na pengine tunaweza kumpandikizia
kipandikizi chenye rekodi zake za matibabu kwa
tahadhari lolote likitokea. Inaonekana ni nzuri. Na kisha mwingine
atasema, Kama inafaa kwa paka wangu,
inafaa pia kwa bibi na babu,
na mtoto wangu mchanga je? Hakuna haja tena ya taarifa
za kupotea mtoto. Hakuna kuhofia
mtoto ataibiwa. Na kisha tutasema, unaona?
pengine SISI sote tuwe nazo.
Na kwenye hicho kipandikizi, tutaweka taarifa ya kila
kitu. Kadi za benki, leseni ya udereva. Fikiria
Tiketi za usafiri. Hakuna haja ya waleti. Fikiri,
huhitaji kubeba funguo tena. Kwa hiyo
swli kila mmoja anayesikiliza atauliza: hilo ni jambo jema?
Kwa sababu huko ndiko tunakoelekea.
Mama Mtangazaji: Ninaisikia kama hadithi vile,
lazima niseme.
Mtangazaji Mwanaume: Ishafika! Iko hapa
Mama Mtangazaji: Najua iko hapa inatumika kwa
mifugo na kidogo kwa binadamu
Mtangazaji Mwanaume: Lakini mtoto wako...
Mama Mtangazaji: Mtoto wako.
Sikiliza
Mch. Anderson: Watu zamani walibaki kushangaa
haya yatawezekanaje?
Unawezaje kumzuia mtu asiuze au kununua
kama hana alama? Lakini tunaona
sasa teknolojia inakuja kasi ambayo itawezesha
kirahisi kabisa kumzuia mtu asinunue
wala kuuza bila kuwa na hii alama. Na unajua?
Watu wengi wana chakula cha kutosha siku
saba tu ndani ya nyumba au chakula cha siku kumi
ndani ya nyumba, kwa hiyo kama huwezi kuuza au kununua
utaumia. Na kimsingi Biblia inasema kwamba patakuwa pia
na sheria itakayosema usipomuabudu mpingakristo
utauawa. Huyu mtu
ni mkuu, anafanya mambo makuu. Anawaleta
watu pamoja. Lakini kwa sharti
moja tu: Kubali au uuawe. Na unaposikia kuhusu
hayo, na unapoyatazama
pengine utasema, Mh, ikiwa hivyo,
nadhani wote tutauawa wale
tunaoamini, wale wamwaninio Kristo.
Nadhani wote tutachinjwa. Na
Biblia inazungumzia kuhusu sisi kuchinjwa. Wote
tutachinjwa. Lakini hili
ni la kuzingatia. Kama hili likiachiwa kuendelea, unasema
kweli, waamini wote watauawa. Kwa sababu
hebu fikiria, angalia teknolojia, angalia
kamera za CCTV zinazowekwa
kila mahali, angalia satelaiti. Sasa hivi polisi wanatumia
vindege vidogo vyenye kamera kuruka
mitaani na kukupeleleza. Ushaziona? Vindege vya
upelelezi. Sasa hivi wanaweka vinasasauti
kwenye mitaani ili waweze kusikiliza unasema nini
Na ni kama vile
kile kitabu cha hadithi za mambo yaliyoharibika cha .
Ndiko nchi yetu inaokelekea, mahali pa
upelelezi kila mahali kwenye jamii. Zamani ilitumika kama
unataka kupanda ndege. Sasa hivi lazima
udhalilishwe na wafanyakazi wa Uwanja wa ndege. Lazima
upitie kwenye skana inakuona mtupu kama ulivyo. Sasa
lazima uskaniwe. Lazime wakupapasepapase.
Lazima uwe na kitambulisho
muda wote na polisi kila mara wanauliza, Wapi
kitambulisho chako? Wapi makaratasi yako? Makaratasi
yako hayajatimia! Na hivo ndivyo nchi yetu ilivyo
sasa. Na hivi
itaendelea mpaka kufikia mahali ambapo huwezi
kukwepa kirahisi gereza hili
dunia. Lakini acha niseme hivi: Hatutauawa wote.
Wengi watauwa, usinielewe
vibaya. Wakristo wengi watachinjwa na kuuawa
kwa ajili ya Kristo. Lakini nitasema
hivi: Hatutauawa wote kwa vile hiyo itafupisha
kipindi hicho. Na Biblia inasema:
(Mathayo :) Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote;
lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
Mch. Anderson: Na Biblia inasema kwamba yote haya
yakiendelea, Yesu Kristo atarudi.
Kumbuka awali tuliongelea kuhusu kurudi kwa Kristo.
Atarudi. Wakati pale
wanapodhani wameushinda Ukristo,
wameshapata serikali yao ya dunia,
wameshapata serikali yao moja ya dunia na Shetani
akiwa ndiye mkuu, Yesu Kristo atakuja mawinguni
na hapo ndipo unyakuo utakapotokeaNna hapo ndipo atakapoanza kumimina
ghadhabu yake kwenye dunia hii. Na unaweza
kuyasoma haya kwenye Ufunuo. Atabadili
maji kuwa damu. Ataunguza miti na nyasi. Atawatuma
nzige toka kuzimu ambao watauma watu kwa mikia
yao iliyo kama nge.
Kama hujakisoma kitabu cha Ufunuo,
Nakushauri sana ukisome. Na usisome
tafsiri mpya (NIV). Soma tafsiri ya awali, ya King James.
Sawa? Na ukitumia muda kusoma,
kwa nini usisome kitu chenyewe kweli? Usikubali
kusoma maigizo. Angalia Sura ya Mstari wa :
(Ufunuo :) Kisha nikaona mnyama akitoka katika
bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu
ya vichwa vyake majina ya makufuru.
(Ufunuo :) Na yule mnyama [mpingakristo]
niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na
miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa
chake kama kinywa cha simba, yule joka[Shetani]
akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na
uwezo mwingi.
Mch. Anderson: Kwa hiyo huyu mnyama anayetajwa,NBiblia inasema joka ndilo lililompa
nguvu zake na kiti chake na kumpa mamlaka.
angalia mstari wa :
(Ufunuo :) Nikaona kimoja cha vichwa vyake
kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake
la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka
kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye
na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa
cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Mch. Anderson: Unaona miezi inarandana na
wakati na nyakati na nusu ya
wakati na siku elfu moja mia mbili na sitini? Waona
mambo haya yote yanavyojipanga? Anasema katika mstari wa :
(Ufunuo :) Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina
lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
Mch. Anderson: Angalia haya. Mstari wa saba.
Ni muhimu sana:
(Ufunuo :) Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda,
akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
Mch. Anderson: Sivyo tulivyoona katika sura ya
mstari wa kwamba lengo la joka lilikuwa ni
kufanya vita na wale wamwaminio Kristo
wazishikao amri za Mungu? Hapa
anasema alipewa ili afanye vita na watakatifu
sikiliza, na kuwashinda.
Nani atakayeshinda vita kati ya watakatifu na ibilisi
katika dunia hii?
Ibilisi. Anasema atafanya vita na watakatifu na
kuwashinda. Kwa mujibu wa
Ufunuo , lengo la mpingakristo ni kufanya vita
na watakatifu. Kwa hiyo hataki
Wakristo wachukue alama ya mnyama ili waepuke
dhiki. Anataka kila Mkristo
afe. Utasema, Mhh, hayo yanasikitisha sana.
Ndiyo hivyo, we soma tu mpaka mwisho wa kitabu na
utaona nani hasa anayeshinda mwishoni. Hili ni
kushindwa kwa mpito tu katika sura ya . Lakini
anasema katika mstari wa :
(Ufunuo : - ) Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda,
akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao
juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha
uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Mch. Anderson: Kwa hiyo huyu mtu anayeitwa mnyama
, huyu mtu ana mamlaka dhidi ya wote
kila kabila na jamaa na lugha na taifa, lengo lake ni
ni kufanya vita na watakatifu na Biblia
inasema kila mtu katika dunia atamwabudu yeye.
Ngoja hapo, Hapana, haisemi. Inasema
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima
cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Hebu nikuulize. Wale ambao
majina yao YAMEANDIKWA katika kitabu cha uzima
nao wanamwabudu? Hapana. Biblia inasema kwamba
atakuwa anaaminika sana na mlaghai sana yamkini
awadanganye wateule. Lakini Mungu
hataruhusu wale waliookolewa kudanganywa
na mtu huyu. Kwa hiyo kila mtu ambaye
ameokoka kweli, hata wale waliokumbwa na mafundisho
ya unyakuo kabla ya dhiki,
watakapoona yanayotokea, au tutumai wakiangalia
kipindi hiki, watabaini kwamba, Ngoja kwanza.
Haya yanatokea. Huyu ndiye mpingakristo.
Sikubali. Siwezi kumwabudu
mtu huyu. Huyu siye Kristo wa kweli. Kwa hiyo yeyote
akataaye kumwabudu atauawa.
Na yoyote asiyemwabudu hawezi kununua
wala kuuza. Huwezi tu kwenda
dukani na kupata alama ya mnyama. Itakuwa siyo
kitu ambacho unaweza
kwenda posta. Nimekuja,
naweza kupata kipandikizi ili niweze kuuza na kununua? Hapana,
Biblia iko wazi. Lazima umwabudu mpingakristo ili
uweze kupokea kipandikizi. Hata miongo
kadhaa iliyopita tayari palikuwa na mashine za kubaini
waongo. Sasa wanatengeneza teknolojia za kuskani ubongo.
Nadhani ili uweze kupata alama ya mnyama, itakubidi
umwabudu mpingakristo na kula kiapo chake
na watajua iwapo unasema ukweli.
Mtangazaji: Hadithi za kufikirika hizi. Kesho ishatufikia.
Mch. Anderson: Si hivyo tu, lakini ukiangalia sana,
usafiri hivi sasa
unadhibitiwa mno. Kuna vituo vya ukaguzi njia kuu
ukiamua kuendesha gari, na ukiamua
kupanda ndege, wafanyakazi wa uwanja wa ndege
watakupitisha kwenye mashine za ukaguzi na
inaonekana vidhibiti vinawekwa kila mahali mradi
usiweze
kufanya lolote kwenye jamii isipokuwa
umemsujudia yule mnyama
na kupokea chapa yake.
Kent Hovind: Sawa kabisa. Tunaelekea kufanyika
maadui. Yesu alisema wazi kabisa
wafuasi wake watachukiwa kwa ajili ya jina lake.
Yeyote asiyeshirikiana na
na hii serikali mpya ambayo wanaipanga ataonekana
ni adui.
Kwa mfano, katika shule, unapoenda kumpeleka
mtoto wako na kumwandikisha shule
wanasema huwezi kumleta asipokuwa amechanjwa
kinga ya magonjwa. Sasa, itakuwaje ikiwa
mwili wako haupatani na chanjo na kusema,
nadhani hizi chanjo zinaweza kusababisha magonjwa ya akili.
Labda inasababisha pia madhara mengine mengi. Sijui,
lakini sitaki kujaribisha. Na
sioni andiko lolote linalofanania na chanjo ambapo
unaweka sumu mwilini mwako ili
kuzuia sumu nyingine zaidi.
Mch. Anderson: Sawa kabisa.
Kent Hovind: Ukweli ni kwamba, mashule yanasema
Huwezi kuandikishwa mpaka umechanjwa
kwa hiyo sasa chagua. Ushikilie imani zako au usujudu na kumpa
chanjo mtoto wako ili asome? Ndivyo itakavyokuwa pia
kwa alama ya mnyama.
Ilikuwa hivyohivyo miaka iliyopita kwa namba
ya Hifadhi ya Jamii. Watu waliikataa
hiyo namba. Aah, Mimi ni jina langu. Na kisha
polepole wakafikia mahali ambapo sasa
kila mtu ana namba hiyo na wala hafikirii mara mbili.
Hiyo ni hatua ya kwanza, pili au tatu
ya kuelekea lengo la mwisho la kuwa na serikali
moja ya dunia?
Mch. Anderson: Shetani anafukuzwa mbinguni.
anajua kwamba ana muda mchache. Anafanya
via na waamini na watakatifu.
Na anafanyaje? Anamuweka
mtu madarakani, sivyo? Joka anampa nguvu.
anampa mtu madaraka
dhidi ya dunia nzima, juu ya kila taifa, jamaa na lugha. Na
mtu huyu atatekeleza vita
ya ibilisi dhidi ya watakatifu. Biblia inasema katika
mstari wa :
(Ufunuo :-) Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa
na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
Naye atumia uwezo wote wa mnyama
yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama
wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
Mch. Anderson: Kwa hiyo huyu mtu anaamrisha aabudiwe.
Inasema katika mstari wa :
(Ufunuo :-) Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka
kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi,
kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia
wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa
na jeraha la upanga naye akaishi.
(Ufunuo :) Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile
sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu
sanamu ya mnyama wauawe.
Mch. Anderson: Utasema, Ni nini hiyo sanamu ya
mnyama iliyopewa
uhai? Kadiri tunavyozidi kukaribia
nadhani tunaweza kuelewa kiaina
teknolojia, kwa hiyo sidhani kama tunaweza
kuelewa wazi kabisa ni aina ipi ya sanamu
itakuwa. Lakini itakuwa ni aina ya sanamu ya mnyama
ambayo inaweza kuongea na kufanya
wengi wasioisujudu wauawe. Hii inanikumbusha
Danieli, sura
ya . Wamkumbuka Nebukadreza aliyekuwa mfalme
wa dunia nzima wakati ule? Wakumbuka
jinsi alivyotengeneza sanamu kubwa na
wakalazimishwa kuiabudu? Nini kilitokea
pale wakikataa kuiabudu? Waliuawa, sivyo?
Haifanani na
tunayoyaona hapa? Hiyo ndiyo picha ya mpingakristo.
Angalia mstari wa . Muhimu sana:
(Ufunuo :-) Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru
kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote
asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya
jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo;
maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Mch. Anderson: Hii ni moja ya zana ambayo Shetani
ataitumia kutesa waaminio.
Kwa hiyo alama ya mnyama ni zana ambayo
itatumiwa kuwapiga vita watakatifu, kwa sababu
ya ukweli kwamba usipoweza kuuza au kununua,
itakuwa vigumu sana kuishi katika
dunia hii ya leo, sivyo? Au katika dunia yoyote. Siyo tu
wanaweka sheria kwamba ikiwa
haumwabudu mpingakristo utauawa.
Na mateso yako pia.
Ndiyo vita dhidi ya watakatifu. Na pia inafanya iwe
haiwezekani kwa watakatifu kununua
au kuuza kwa kuwa hawana alama ya mnyama,
na alama ya mnyama ndiyo
kitu pekee kitakachotolewa kwa wale wamwabuduo
mnyama. Na wale waliookolewa, wale
watakatifu, hawatamwabudu mnyama. Biblia iko wazi
kwenye hilo katika Mathayo
na kwingineko. Kwa hiyo hawataweza kuuza wala
kununua na watakuwa na
hukumu ya kifo juu yao. Hebu jifikirie uko kwenye
dunia na sikusema
nchi, sikusema taifa, nimesema
DUNIA ambako huwezi kununua
wala kuuza na ambako pana hati ya wewe uuawe. Unaweza kuona
itakavyokuwa vigumu kuishi katika dunia ya namna
hiyo? Siyo tu hivyo, unaonaje kuhusu
kamera zote za upelelezi ambazo ziko?
Au zile kamera zinazoweza kusoma namba za magari?
Au zile kamera za ukaguzi wa mwili? Au kuonyesha vitambulisho katika vituo vya ukaguzi? Kuonyesha
kitambulisho kabla ya kupanda treni? Kuonyesha kitambulisho kupanda ndege? Wajua hayo?
Muda si mrefu utalazimika kuonyesha kitu kingine. Sawa, tuonyeshe
mkono wako wa kuume. Hapo sawa, unaweza kwenda.
siku njema. Haya si ya kufikirika tu. Labda
watu watakapokuwa wakiyasoma haya miaka mia chache
iliyopita hawakuweza kuona kama vile
sisi tunavyoona. Tunapoangalia, tunayaona yana
kauzito jamani, sivyo?
Ndiyo maana nadhani tuko karibu.
Wakristo wa leo hawako tayari kwa haya
hata kidogo. Hawako tayari kabisa. Unajua
unatakiwa ufanye nini? Unatakiwa kujiandaa
mwenyewe kiroho na kuwa tayari, usije ukashangaa
Nini kinatokea?
Uwe tayari. Unahitaji kujiandaa. Ndiyo maana Mungu
anatuonya na kuuonya na
kutuonya na kutuonya. Ndiyo maana hata Paulo
aliwaonya watu wa siku zake. Ni wazi
hawakuwa wakiishi katika siku za dhiki kuu, lakini
walikuwa wakipitia katika
dhiki kama kila mwamini anavyopitia. Alisema,
Tuliwaonya. Amin, wakati
tulipokuwa nanyi, tuliwaambia kwamba tutapitia dhiki
kama ilivyokuja kutukia,
kama mjuavyo. Na hivyo tunahitaji nasi kujihadhariNna kuelewa kwamba haya yanakuja ili kwamba
tuweze kuyamudu.
Ronald Rasmussen: Wakristo wa leo hawaonywi
kuhusu matukio haya watakayoyakabili
katika dhiki kuu. Badala yake, wachungaji
katika Marekani yote wanafundisha washirika wao kwamba
unyakuo utatokea kabla ya mpingakristo hajaanza
vita yake dhidi ya watakatifu na kwamba
unyakuo ndio utakuwa tukio la kwanza kabisa la
mfululizo wa matukio yaliyotabiriwa ya Mungu. Mafundisho haya
yajulikanayo kama ukaribu, hufundisha kwamba Kristo anaweza
kurudi mawinguni muda wowote na kwamba
hakutakuwa na dalili ya kurudi kwake. Hata hivyo,
Biblia inafundisha kwamba kurudi kwa Kristo
hakutokei muda wowote na kwamba pana matukio
ambayo lazima yatokee kwanza.
Mch. Anderson: Inawezekana ushasikia kuhusu mafundisho haya yasemayo Yesu anaweza kurudi leo.
Nani ashayasikia? Huitwa Kristo kurudi muda wowote. Wanaamini kwamba
Yesu atarudi muda wowote. Nimewauliza watu mara nyingi waniambiapo
Yesu anaweza kurudi muda wowote, Wapi Biblia inaposema hivyo? Na kile ambacho
hunijibu ni, Biblia inasema hakuna mtu ajuaye siku wala saa
atakayorudi. Na mara nyingi hawawezi kukuonyesha na inabidi uwasaidie
kuupata huo mstari. Na husema, Sawa, sinao huo mstari mbele yangu. Sijui unasema nini hasa
wala sura yake. Lakini najua ya kwamba Yesu alisema kwamba hakuna mtu aijuaye siku wala saa. Nami husema,
Acha nikusaidie. Alisema hayo katika Mathayo :. Acha nikusomee yale Biblia
inasema, kwa vile nataka kukuonyesha ni namna gani mafundisho haya ya Wakristo wengi hayatokani na Biblia.
Ukienda kwenye duka lolote la vitabu vya Kikristo, utakuta kila aina ya vitabu
na video na ushaisikia hii filamu Left Behind? Hadithi tupu.
Haihusiani kabisa na Biblia. Nje kabisa ya Biblia.
Na Biblia inasema katika Mathayo ::
(Mathayo :) Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye,
hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Mch. Anderson: Kwa hiyo watu huchukua mstari huo na kusema, Unaona? hakuna mtu
aijuaye siku wala saa. Hiyo ina maana inaweza kutokea muda wowote. Lakini angalia
alisema, Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye. Kwa hiyo swali la kujiuliza ni,
Siku ipi? Ni siku ambayo alimaliza punde kuizungumzia
Iko hivi.
Ukirudi nyuma mpaka mstari wa , anasema siku hiyo ni baada ya dhiki kuu. Anasema katika mstari wa :
baada ya dhiki ya siku zile,
Mch. Anderson: Anaelezea matukio yatakayokuja kutokea. Kisha anasema:
(Mathayo :) Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni,
Mch. Anderson: Kwa hiyo hatujui siku waa saa lakini jambo moja tulijualo ni kwamba
itakuwa baada ya dhiki kuu. Wale watu waaminio unyakuo kabla ya dhiki ndio huchezesha
mawazo yao sarakasi ukiwaonyesha mstari, Unauona, unasema wazi hapa BAADA YA
DHIKI. Hiki ndicho watajibu,
Hiyo siyo kuhusu unyakuo.
Huo siyo unyakuo. Ukiwauliza, Mnajuaje? Ni kwa kuwa ni baada ya
dhiki. Na tunajua unyakuo ni kabla ya dhiki.
Lakini ukiwauliza, Sawa, ni wapi Biblia inasema unyakuo unaweza
kutokea muda wowote? Ni hapahapa, inasema hakuna mtu ajuaye siku wala saa.
Lakini umesema sasa hivi tu hii haikuwa inazungumzia unyakuo. Hivo inaposema kuhusu dhiki,
Mathayo haizungumzii unyakuo. Lakini inaposema hakuna mtu ajuaye siku wala
saa, ghafla Mathayo inazungumzia tena kuhusu unakuo. Na inaposema watu wawili
watakuwa kondeni, mmoja atwaliwa na mwingine aachwa, hapo tena inazungumzia unyakuo. We
funga domo lako fanya uambiwayo. Funga domo lako na uamini unyakuo kabla ya dhiki kwa vile
nshasema hivyo. Utasema, elezea pande zote. Tenda haki kwa pande zote. Sawa, huu hapa
upande mwingine. Funga domo lako na uamini yale niliyokuambia na acha kuuliza maswali.
Funga mdomo wako na uamini kwa vile nimeshasema hivyo. Huo ndio upande wa unyakuo kabla ya dhiki.
Ni kweli hawana kitu. Nimeenda andiko kwa andiko baada ya andiko, na wao wametengeza
mafundisho mazima kutoka pasipo kitu. Angalau mafundisho mengine ya uongo huegemea mistari fulani ya Biblia ambayo
imetoholewa na watu hutumia mistari ya Biblia na kuinukuu vibaya.
Unyakuo kabla ya dhiki haunukuu vibaya andiko lolote. Hauna hata
andiko moja. Hakuna andiko lolote lisemalo chochote kuhusu unyakuo kutokea
kabla ya dhiki. Ni mafundisho yasiyotokana kabisa na maandiko
yoyote. Yanatokana na mapokeo. Yanatokana na kitabu au jedwali ambalo mtu fulani alisoma.
Haitokani na Biblia. Haikutoka kwenye Biblia. haina
asili yake kwenye Biblia. Kila ninapoyaeleza haya kwa washirika,
hawana tatizo kulielewa hili fundisho. Ni wahubiri ndio walio
shikilia fundisho hili, na nitakuambia kwa nini.
unyakuo kabla ya dhiki ni fundisho mashuhuri.
Ukitaka umashuhuri, lazima ufundishe unyakuo kabla ya dhiki. Ukianza
kufundisha unyakuo unakuja baada ya dhiki, utatengwa,
utasemwa vibaya, na utakataliwa kwenye huduma, kwa vile
hawataki kubadili mafundisho haya.
Kwa sababu wapo watu huko ambao
wana ajenda ya kuhakikisha hakuna mtu anayesikia ukweli kuhusu mafundisho haya. Ndivyo. Na
vile wanavyoendelea kubakiza mafundisho haya gizani ni kupitia hofu na vitisho. Naongea
na wachungaji muda wote. Nawaonyesha ukweli wa haya. Wanakubaliana nami. Lakini
hawawezi kwenda madhabahuni na kuhubiri mafundisho haya, kwa vile wanaogopa wachungaji
wenzao wote watawachukia. Hawatapata mialiko ya kuhubiri.
Hawataenda kuhubiri katika makanisa yao kwa vile inabidi
uamini unyakuo kabla ya dhiki ile uwe kwenye klabu. Na kama hauamini hayo, hauwi. Mara
nyingi hawakubali mafundisho haya kwa vile wanaona aibu kugeuka sababu wamekuwa
wakifundisha visivyo miaka yote hii. Na hawataki kukiri hayo. Hawataki
kukiri kwamba vyuo vya Biblia viliwafundisha visivyo. Hawataki kukubali kwamba wao
walifanya makosa. Kila mtu hufanya makosa.
Wote tunakua. Tunajifunza vitu vipya. Kama
umekosea kitu fulani, unarekebishwa. Biblia inasema katika Wagalatia ::
(Wagalatia :) Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama
ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Mch. Anderson: Wahubiri hawa inabidi wachague
kama kupendeza watu ni bora zaidi, kwa
kuhubiri watu wanachokipenda, kuhubiri unyakuo kabla ya dhiki kwa vile ndivyo kila mtu
anataka kukisikia, sababu wamependa ile filamu
na wana michezo ya video na ya mezani
na DVD, au wachague kusema kile hasa Biblia
inachokisema na kusimama na kuhubiri kwamba
unyakuo unakuja baada ya dhiki. Ni mfano mzuri wa watu kuchukua kile watu
wanasema na siyo Mungu anachosema. Ni mfano halisi wa mfano wa kutofanya Biblia ndio
mamlaka ya mwisho na kwenda na mapokeo, kwenda na uliyofundishwa, kwenda na
wasemacho watu, kufuata mkumbo, badala ya kwenda na kile Biblia inakisema.
Mch. Jimenez: Nilikuwa naamini unyakuo kabla ya dhiki. Ndicho nilichofundishwa tangu
nikiwa mtoto na kwa kweli huwezi kuhoji yale uambiwayo, lakini nilipouona
ukweli na kuanza kuona maandiko yenyewe na mafundisho hasa Biblia yenyewe inayotoa
binafsi niliamua kuchagua ama niendelee kufuata mkumbo au
Nitaendelea kufuata ya watu, au kama nitasimamia kile nikiaminicho
na kusimamia kile nikijuacho kuwa ni kweli. Katika maisha yangu nimeshambuliwa na
watu wakinisema vibaya kwa sababu tu ya msimamo wangu kuhusu unyakuo wa kabla ya dhiki,
lakini natumai kwamba labda wewe unayenisikiliza au unayeniangalia au unaanza
kuuona ukweli wa haya, kwamba utasimamia imani na
kushikilia msimamo na pengine kutusaidia kuweza kubadili watu wawe kinyume na mafundisho hayo
yasiyotokana na maandiko ya unyakuo kabla ya dhiki kuu.
Kent Hovind: Mstari mwingine muhimu ulionipata ni ule wa Thesalonike :-
( Wathesalonike :-) Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu
Kristo [anarejea ukweli kwamba Bwana Yesu Kristo yuaja], na
kukusanyika kwetu mbele zake, [likimaanisha unyakuo],kwamba msifadhaishwe upesi
hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba
siku ya Bwana [akimaanisha unyakuo] imekwisha kuwapo.
Mch. Jimenez: Anasema, Angalia, haujakuwapo. Siyo tukio lijalo ambalo
litatokea. Anasema, mtu asiwadanganye kwa namna yoyote kwamba ile siku (anazungumzia
siku ambayo tutakusanywa pamoja)
haitakuja isipokuwa mpaka uje ukengeufu
kwanza, akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu. Hapo imethibitishwa
kwenye maandiko kwamba siku ya kukusanywa kwetu pamoja na Bwana Yesu Kristo
haiji mpaka ukengeufu na mtu wa kuasi vifunuliwe. Kitu pekee
ambacho kinaweza kutokea muda wowote ni ukweli kwamba mpingakristo yuaja.
Mch. Anderson: Kwa hiyo Biblia inasema bila kupindisha kwamba siku ya kuja Kristo haitokei muda wowote tu.
Anasema, kama kuna mtu akikwambia siku ya Bwana i karibu, mtu huyo
anakudanganya. Mtu huyo ni mwongo. Anasema usidanganyike kwa neno au kwa
roho au hata kwa waraka unaoonekana kutoka kwetu, waraka unaosemekana umetoka kwetu tukisema
siku ya Kristo i karibu. Usiache mtu yoyote kukudanganya kwa namna yoyote. Hiyo siku haiji isipokuwa
X, Y, na Z zitokee kwanza. Unyakuo hauwezekani kabisa kutokea muda wowote. Dhiki
lazima itokee kwanza. Mpingakristo lazima awe madarakani kwanza. Jua na mwezi
vitiwe giza kabla ya siku ile kuu na ya kutisha ya Bwana haijafika. Biblia
iko wazi kabisa. Siku hiyo haiji isipokuwa ukengeufu na yule mtu
wa uharibifu wafunuliwe. Mpingakristo atakaa hekaluni
mwa Mungu na kujitangaza kuwa ndiye Mungu. Mpingakristo atakuwa madarakani kabla ya unyakuo
kutokea. Ni rahisi hivyo. Lakini ukiangalia Luka , inakuja kimpangilio
kabla ya Mathayo , sababu Mathayo ni sura pacha ya Luka . Kwa hiyo katika Luka
tunasoma tukio la awali kabisa kuandikwa
Yesu akiwafundisha wafuasi wake mafundisho haya. Biblia inasema:
(Luka :) Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake
Mwana wa Adamu [Yesu Kristo].
Mch. Anderson: Watu wengi huchukua andiko hili na kusema kwamba hii ina maana watu
watakuwa waovu kama walivyokuwa wakati wa Nuhu. Pia, alisema kama ilivyokuwa
katika siku za Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake Mwana wa Adam.
Na watu watasema, Ndiyo, watakuwa waovu tu kama ilivyokuwa katika Sodoma na Gomora.
Na watakuonyesha mambo yote yanayoendelea katika jamii yetu yafananayo
na yaliyokuwa yakitokea Sodoma na Gomora. Na watasema alimaanisha watakuwa waovu
kama ilivyokuwa Sodoma na Gomora au waovu kama wakati wa Nuhu
Lakini kiukweli, huo si ulinganisho Yesu anaouweka.
Mch. Jimenez: Kwenye mstari wa anasema:
(Luka :-) Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa,
walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka
Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
Mch. Jimenez: Tunachojifunza kutoka kwenye vifungu hivi ni kwamba Lutu alitolewa
kutoka Sodoma, hiyo ndiyo picha ya unyakuo.
Unawaona malaika wawili wakienda Sodoma ambao
wanawakilisha dunia na kutolewa kwa waamini kabla ghadhabu ya Mungu haijamiminwa
kwenye mji. Kitabu cha Ufunuo kinafundisha kitu kilekile. Biblia inasema katika kitabu
cha Ufunuo kwamba Bwana Yesu Kristo atawatuma malaika kuwakusanya waamini na
kuwatoa ulimenguni. Kitabu cha Ufunuo wazi kabisa kinatuambia nusu saa itapita
kabla hajaanza kumimina ghadhabu yake.
Mch. Anderson: Huu mfumo wa Left Behind ambamo kila mtu anapotea na kila mtu
anashangaa, Wameenda wapi? Hicho sicho watu watakachokuwa wakikisema. Sababu
Biblia inasema siku hiyohiyo tutakayonyakuliwa, Mungu ataanza
kumimina hukumu. Mungu ataanza kunyesha moto na kibiriti kwenye dunia hii. Watu
watajua kuna kitu kinatokea. Watu watakimbia wajifiche.
Watu watiambia milima iwaangukie na kuwaficha sababu
ya moto, kibiriti, ghadhabu itakayokuwa inakuja. Siku hiyohiyo ambayo tutanyakuliwa
ndiyo siku hiyohiyo ambayo Mungu ataanza kumimina ghadhabu yake. Ndiyo maana
pale jua na mwezi vitiwapo giza, Biblia inasema siku ile ya kutisha imekuja na
ni nani awezaye kustahimili? Kwa sababu siku ileile, nusu saa baadaye, Mungu ataanza kunyesha
moto na kibiriti. Kwa hiyo sura ya sita ya Ufunuo, jua na mwezi vinatiwa giza, Sura ya saba
mkutano mkubwa wa waamini unatokea mbinguni. Sura ya nane, anaanza kumimina
ghadhabu yake. Sawa kabisa na kile Biblia inafundisha katika Mathayo . Jua na mwezi kutiwa giza,
kisha unyakuo. Ni rahisi hivyo. Niongeapo na watu waaminio unyakuo kabla ya dhiki
huniambia moja ya mambo mawili. Ama huniambia kwamba
unyakuo wala hata haujatajwa katika kitabu cha Ufunuo jambo ambalo ni la kushangaza
kusema kwa vile kitabu cha Ufunuo kinaeleza kwa kina matukio ya mwisho
wa dunia. Kuacha tukio muhimu kama vile Yesu Kristo kuja mawinguni na
waamini wote wa umri wote kunyakuliwa pamoja naye mawinguni
hilo ni tuko kubwa. Kusema kwamba halikuandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo
na kwamba halipo kabisa katika kitabu cha Ufunuo, haifikiriki. Lakini kwa vile
inachekesha sana kusema kwamba unyakuo haumo kwenye kitabu cha Ufunuo,
wengi wanyakuo-kabla-dhiki wamejaribu kutafuta kitu mbadala ambacho
wanaweza kukitumia kama unyakuo ambao ni kabla ya dhiki kuu, na hiki ndicho nikisikiacho
mara kwa mara Ufunuo :. Ufunuo : unasema:
(Ufunuo :) Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na
sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda
hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
Mch. Anderson: Kwa hiyo hii sauti ni kama tarumbeta. Hakuna tarumbeta katika mstari huu
sambayo inaongea na kusema na Yohana (mtu mmoja), Panda huku nami
nitakuonyesha WEWE mambo ambayo hayana budi kutukia baada ya haya. Nao husema, Unaona? huo ndio unyakuo
wazi kabisa. Mtu mmoja akichukuliwa. Wanasema ndio unyakuo. Cha kuchekesha
zaidi ni kwamba hata hawasomi mstari wa . Kwa sababu mstari wa inasema:
(Ufunuo :) Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa
mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;
Mch. Anderson: Unyakuo siyo roho kuenda Mbinguni. Unyakuo ni ufufuo wa mwili
Tutanyakuliwa na miili yetu kwenda hewani. Huu siyo
tu kitu ambacho roho inaenda juu. Biblia iko wazi kwamba unyakuo siyo fumbo,
ufufuo wa miili ya waliokuwa katika Kristo ambao watafufuka kwanza. Kisha sisi tuliohai
na kusalia tutanyakuliwa kwenda pamoja naye katika miili yetu. Hivyo huu unyakuo wa roho
ya mtu mmoja, Yohana, ni wazi siyo unyakuo. Na kama ukidhani huu ndio
unyakuo, umechukua tafsiri potofu. Inachekesha kwa vile watu
niongeao nao wanaoamini unyakuo kabla ya dhiki wanadai kuisoma Biblia kama ilivyo.
Lakini ukiwauliza wakuonyeshe unyakuo katika Ufunuo, watakupeleka Ufunuo
:. Mtu mmoja akipelekwa mbinguni. Hata hawasomi mstari wa pale asemapo,
Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni. Wala hata
hakuenda na mwili wake. Mwili wake ulibakia hapahapa katika Kisiwa cha Patmo. Waliokufa katika Kristo
watafufuka kwanza. Kisha sisi tuliohai na kusalia tutakutana nao
mawinguni. Hizi siyo roho zikutanazo. Hii ni
miili halisi. Ni kupindisha maneno kusema kwamba huo ni unyakuo. Wale ambao
wanaamini katika unyakuo kabla ya dhiki inabidi waseme Ufunuo : ni unyakuo
kwa sababu ndicho kitu pekee wanachoweza kukipata katika kitabu cha Ufunuo kabla
ya dhiki kuu. Na haienei. Inabidi watafute kitu chochote tu, nadhani. Nilikua
nikifundishwa unyakuo kabla ya dhiki. Na nilipozidi kukua, nilifundishwa kwamba
hautajwi kabisa kwenye kitabu cha Ufunuo. Siku zote nilidhani pana tatizo mahali
Tukio muhimu na kubwa kama unyakuo na una kitabu kinachohusu
unabii wa siku za mwisho, kitabu cha Ufunuo, na kisikitaje? Haileti
maana yoyote. Siku zote nilifundishwa utotoni kwamba unyakuo utatokea wakati unaendelea
na shughuli zako za kila siku na ghafla unapotea. Lakini kubwa zaidi
kwa vile Biblia inasema kila jicho litamwona. Tutaona jua
na mwezi vikitiwa giza. Inasema kwenye Luka kwamba muonapo vitu hivyo mjue mwisho
umekaribia, akasema kesheni, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia. Hebu fikiri nini
itakavyokuwa wakati jua linatiwa giza, na mwezi unatiwa giza, na nyota zinaanza kuanguka,
na tukiviona tujue ndio hivyo. Mwisho umefika. Tumeweza kuufikia.
Ni kama ufunguzi wa Kihollywood. Wakati watu
mashuhuri wakifika popote. Utaona mataa yakimulika na sauti nzito zikirindima na
moshi na kila kitu kingine. Wanataka kujionyesha kwa watu. Jamani ee, niangalieni. Kama
ukiisoma Ufunuo sura ya au Mathayo , Marko au Luka , au vifungu vyovyote ambavyo
vinaelezea jua na mwezi kutiwa giza, vinasisimua kweli kuviangalia. Jua
na mwezi kutiwa giza kutamfanya kila mtu duniani afahamu.
Lakini pia inasema kutakuwa na matetemeko, kwa hiyo kama ni kipofu,
nayo yatakufanya ufahamu.
Mch. Anderson: Na katika wakati wa kiza hicho kikuu, Yesu Kristo atakuja
mawinguni, akimulika anga lote. Biblia inasema atamulika anga kama vile radi
imulikavyo toka upande mmoja wa mbingu hadi mwingine, na tutazamapo juu na tutamuona
Yesu Kristo akija na mawingu. Tutajua kwamba wakati wowote tutanyakuliwa
tuende kuwa pamoja naye. Napenda niwe hai kuiona siku hiyo. Sijui iwapo itatokea
wakati wetu wa maisha. Natamani itokee wakati wa uhai wangu. Natumai nitaweza
kuhimili dhiki kuu na udhia. Ni furaha iliyoje kuwa hai siku hiyo
ambayo Yesu Kristo yuaja na mawingu.
Ni kuu mno kuliko tulivyofanywa tuamini itakuwa.
Kent Hovind: Wazo kwamba kutakuwa na unyakuo wa siri ambapo watu
baadaye itabidi watafute kumetokea nini. Si kweli kabisa.
Atafanya kila mtu ajue kwa ufunguzi wa Kihollywood.
Mch. Anderson: Unasema kweli kabisa. Katika Ufunuo Sura ya inasema Tazama,
yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona. Neno 'yuaja' laonyesha wakati unaoendelea.
Hivyo huo ni wakati mwingine yuaja. Yuaja na mawingu na kila jicho litamwona
Ni wazi kabisa. Kwa wasiookolewa hili litawatisha kiasi cha kufa. Biblia
inasema kwamba wamwonapo akija na mawingu, wataanza kulia,
watalia machozi, wataogopa sana. Lakini akina sisi ambao
tutakuwa tunasubiri kurudi kwake, tutafurahi furaha kuu, tutachangamka, na
itakuwa ni raha kuu kujua mwisho umefika.
Mch. Jimenez: Binafsi natamani filamu hii ifanikiwe. Natamani kuona filamu hii
inatumiwa na Mungu kuwafungua watu macho wauone ukweli. Nadhani ni
muhimu sana turudi kwenye Biblia. Nakumbuka nilipokuwa kijana na
nikikua, sikupenda hata kukisoma kitabu cha Ufunuo kwa vile nilidhani
sikielewi au kila nikisoma kitu fulani niliuliza,
Ndiyo hiki kweli inakisema? Inamaanisha hiki kweli? Nilipoweza kujua
ukweli kuhusu unyakuo, ulinifungulia maandiko. Napenda kusoma kitabu
cha Ufunuo siku hizi. Na kadiri nikisomavyo, kinazidi kuleta maana. Nadhani kwamba
kama tukiweza kufikia jamii za Wakristo, jamii za kihafidhina,
jamii za Wabaptisti, na tukaweza kuwafunua macho yao kwa jambo hili, hapo
pengine tutaweza kuleta kupenda neno la Mungu na uamsho wa neno la Mungu na
uamsho wa kusoma neno la Mungu kwenye madhabahu za nchini kwetu, na tungeweza kweli
kuona kazi kubwa ikifanywa kwa ajili ya Mungu.
Mch. Anderson: Sababu iliyotufanya tutengeneze filamu hii siyo kuleta tu ubishi wa mafundisho au tu
kumkosoa mtu fulani ambaye mtazamo wake khusu unabii wa Biblia una tofauti kidogo na wetu. Hilo
siyo lengo letu. Haya matukio ni matukio halisi ambayo yatatokea. Biblia inatuambia PATAKUWA
na serikali moja ya dunia. PATAKUWA na dini moja ya dunia. PATAKUWA na
sarafu moja ya dunia. Haya si nadharia za kijuha ambayo watu wanaweza kupuuzia. Haya ni matukio
ambayo kikweli kabisa yatakuja kutokea. Watu watauliwa kwa wingi. Patakuwa na
baa la njaa. Patakuwa na tauni. Patakuwa na udhia.
Patakuwa na vitu ambavyo dunia hii haijawahi kuvipitia na Wakristo
hawajajiandaa kabisa. Kwa sababu waliamini masimulizi ya uongo ya unyakuo kabla ya dhiki.
Naamini katika unyakuo. Ni mafundisho ya Kibiblia. Lakini unyakuo unakuja
BAADA ya dhiki.
Mch. Jimenez: Utaniambia, Mch. Jimenez, kwani haya yana umuhimu wowote? Huu ndio umuhimu wake.
Kwa mafundisho ya unyakuo kabla ya dhiki naamini hakuna umuhimu wowote wa
kuzingatia nini tunafanya. Kwa vile, lolote tufanyalo ni ama nitakufa kwa amani uzeeni
au nitaendelea na maisha yangu, nikienda likizo, nikiwekeza kwenye pensheni,
nikiishi maisha mazuri, na siku moja ghafla nitapotea, kabla ya jambo lolote baya kutokea.
Mafundisho haya yanafundishwa kwa mamilioni ya watu naamini yametufanya tuwe
wavivu sana na tulioridhika na Ukristo wetu. Tunahitajika kuhubiri injili. Inatubidi
tuende huku na kule. Lazima tuwaelimishe watu na kuwaambia, Jamani, pana udhia unakuja.
Nenda likizo na kufanya yote ufanyayo, lakini
jiimarishe utu wa ndani. Ni vema ukichukua Biblia yako. Ni vema ukaanza kujifunza
Biblia. Ni vema ukaanza kutembea na Mungu na kumfahamu Mungu. Ni vema ukaanza kusoma
Biblia, kwa vile itafika siku watakayokuondolea Biblia hii. Leo hii
tuna uhuru kamili wa kukutanika, wa kufungua Biblia, wa kulihubiri neno, lakini
panaweza kuja siku ambayo mkutano huu utakuwa ni kinyume cha sheria, wakati Biblia hii itakuwa
imepigwa marufuku, wakati kufanya tunachokifanya sasa kutakuwa ni uhalifu. Kama tukimpenda
Mungu, lazima tuwafikie watu kwa injili ya Yesu Kristo.
Mch. Anderson: Yote hayo ni kusema hivi. Mambo haya niliyowahubiria ili kwamba
usije ukakwazika. Wakati udhia ukija, au wakati ukitakiwa kuchukua alama ya mnyama
kwenye mkono wako wa kuume au kwenye paji la uso, utakumbuka mahubiri haya. Au pengine hayatatokea
wakati wa uhai wetu, au labda yatatokea. Lakini yakitokea, kumbuka ibada hii. Ndiyo
maana Yesu alisema haya na ndio maana nayasema. Utasema, Haya ni kututisha? Hapana,
Biblia inasema duniani mnayo dhiki. Unakereka? Hapana. Anasema
dunani mnayo dhiki, lakini jipeni moyo. Mimi nimeushinda ulimwengu.
Jipeni moyo. Msivunjike moyo. Usitoke nje ya ibada, Ah, unamaanisha haya?
Kuchinjwa? Vifungo? Njaa? Magonjwa? Unasema kweli? Hapana, jipeni moyo. Yeye
ameushinda ulimwengu. Labda itatokea wakati wa maisha yetu, labda haitatokea. Lakini vyovyote
vile, Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye kinyume chetu? Bwana Yesu Kristo asifiwe. Tuinamishe vichwa vyetu
na kuomba. Baba, tunakushuru sana kwa ukweli ulio wazi kwenye neno lako
na tunakushukuru sana kwa kutupa Roho Mtakatifu atuongoze. Nisingeweza
kufahamu haya yote mimi mwenye ukizingatia mafundisho ya uongo niliyopokea kwa
watu walionidanganya na Scofield, lakini asante kwa Roho Mtakatifu katika chumba kile
miaka mingi iliyopita aliyeyakata yote hayo na kuandika maneno haya matatu mawazoni mwangu.
Maneno haya matatu yalithibitishwa mawazoni mwangu toka Mathayo nikiwa mvulana wa miaka : BAADA YA DHIKI
Nawaombea wote ambao maneno haya yataingia mioyoni mwao na mawazoni mwa kila mtu aliyeko hapa
jioni hii. Tunakupenda na kukushukuru na katika Jina la Yesu tunaomba, Amen. Tuimbe
wimbo mmoja mfupi kabla hatujaondoka.
WIMBO: Nionapo Amani Kama Shwari
Mch. Jimenez: Huu wimbo naupenda sana, na tunaenda kuimba beti nilipendalo
sasa. Mara nyingi unapoimba wimbo unaanza tu kuimba. Huna
muda wa kutafakari maneno yake na unachosema. Angalia maneno ya beti la tatu la wimbo huu.
Linasema, Dhambi zangu zote wala si nusu
Zimewekwa msalabani
dhambi zangu zote wala si nusu? Angalia lisemacho. Linasema
zimewekwa msalabani, wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu.
Yatafakari maneno hayo wakati ukiimba. Tuliimbe beti hili, tukijiandaa kwa
mahubiri.
Dhambi zangu zote, wala si nusu
Zimewekwa Msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu!
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.
Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.
Biblia iko wazi kabisa kuhusu wokovu. Hautegemei
mwema kiasi gani. Watu wengi
wanadhani ni wema sana na wataenda mbinguni
kwa sababu ya wema wao.
Lakini Biblia inasema, kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa utukufu wa Mungu.
Biblia inasema, Kama ilivyoandikwa, hakuna mwenye haki hata mmoja. Mimi siyo mwenye haki.
Wewe si mwenye haki. Na kama wema wetu ndio ungetupeleka mbinguni,
hakuna hata mmoja wetu angeenda.
. Kiri kwamba wewe ni mwenye dhambi.
Biblia inasema hivyo hata katika Ufunuo ::
(Ufunuo :) Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi,
na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na [sikiza kwa makini] waongo WOTE, sehemu yao
ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Nimeshawahi kusema uongo. Kila mtu ashawahi kusema uongo. Wote tumefanya dhambi,
tumefanya mambo mabaya kuliko kusema uongo. Lazima tukubali. Wote tunastahili jehanamu.
. Tambua adhabu ya dhambi.
Lakini Biblia inasema:
(Warumi :) Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo
alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Hivyo Yesu Kristo, kwa vile atupenda sisi, alikuja katika dunia hii. Biblia inasema Mungu
alifanyika mwili. Kimsingi Mungu alichukua umbo la binadamu. Hakutenda dhambi.
Hakufanya dhambi yoyote. Lakini walimpiga na kumtemea mate na kumsulubisha msalabani.
Biblia inasema alipokuwa hapo msalabani, alibeba dhambi zetu zote kwenye mwili wake
msalabani. Kwa hiyo kila dhambi uliyowahi kuifanya, dhambi yoyote niliyowahi kuifanya, ilikuwa
kana kwamba Yesu ndiye aliifanya. Aliadhibiwa kwa dhambi zetu. Kisha, waliuchukua mwili wake
alipokufa na kuuzika kaburini, na roho yake ilienda kuzimu kwa siku tatu na
usiku na mchana (Matendo :). Siku tatu baadaye, alifufuka. Akajionyesha kwa
wafuasi wake alama za misumari. Biblia iko wazi kabisa kwamba Yesu alikufa kwa
ajili ya kila mtu. Inasema kwamba alikufa siyo tu kwa ajili ya dhambi zetu, bali pia dhambi za
ulimwengu mzima. Lakini pana kitu lazima tukifanye ili tuokolewe. Biblia inalo swali hilo
katika Matendo : Nifanye nini nipate kuokolewa? Nao wakajibu:
(Matendo :-) Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Hayo tu. Hawakusema, Jiunge na kanisa utaokolewa. Batizwa
utaokolewa. Ishi maisha mema utaokolewa. Tubu dhambi zako zote
na utaokolewa. Hapana. Alisema, Amini.
. Amini kwamba Yesu alikufa, akazikwa, na
akafufuka kwa ajili yako.
Hata mstari mashuhuri kuliko yote kwenye Biblia nzima, ambao umeandikwa chini ya kikombe
cha OutBurger, ni mashuhuri sana kiasi kila mtu ashausikia: Yohana ::
(Yohana :) Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Milele ina maana ya milele. Inamaanisha milele. Yesu akasema:
(Yohana :) Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala
hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Biblia inasema katika Yohana ::
(Yohana :) Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
Ukimuamini Yesu Kristo, Biblia inasema utakuwa na uzima wa milele.
Utaishi milele. Huwezi kupoteza wokovu wako. Ni wa milele. wa milele.
Ukishaokolewa, mara ukimwamini Yeye, umeokolewa milele, bila kujali lolote lingine,
hauwezi kuupoteza wokovu wako. Hata kama utaenda kufanya dhambi fulani ya kutisha,
Mungu ataniadhibu katika dunia hii. Nikienda nikaua mtu leo hii, Mungu
atahakikisha naadhibiwa. Nitaenda kifungoni au matokeo mabaya zaidi au
nitahukumiwa kifo, au lolote lile dunia hii itaniadhibu. Mungu atahakikisha
ninaadhibiwa zaidi. Lakini siendi motoni. Hakuna
kitu ninachoweza kukifanya mpaka niende motoni. Nimeokoka. Na nikienda motoni, Mungu mwongo,
kwa sababu aliahidi kwamba kila amwaminiye Yeye anao uzima wa milele. Alisema:
(Yohana :) naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.
Ndiyo maana pana mifano mingi ya watu kwenye Biblia waliofanya mambo mabaya
sana, lakini walienda mbinguni. Kwa vipi? Kwa sababu walikuwa wema sana? Siyo. Kwa sababu
walimwamini Bwana Yesu Kristo. Dhambi zao zilisamehewa. Watu wengine walioishi
maisha mema zaidi machoni pa dunia, au kweli walikuwa wema zaidi, lakini
hawakumwamini Kristo, wataenda motoni kuadhibiwa kwa dhambi zao.
. Mwamini Kristo tu kama mwokozi wako.
Acha nifunge kwa fikra hii, jambo moja nililotaka kulizungumzia
leo hii. Palikuwa na swali Yesu aliulizwa na mmoja wa wanafunzi wake. Swali hilo
lilikuwa: Wanaookolewa ni wachache? Hio lilikuwa swali zuri, sivyo? Wanaookolewa ni wengi?
Au ni wachache wanaookolewa? Wale wanaodhani watu wengi wa dunia hii wataenda
mbinguni? Unajua alijibu nini? Alisema katika
Mathayo :
(Mathayo : - ) Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana,
na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Akaendelea na kusema hivi:
(Mathayo :-) Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia
katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako
kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Kwanza kabisa, walio wengi dunia humu hata kusema tu wanamwamini Yesu hawasemi.
Angalau wengi kwenye darasa hili wanadai wanamwamini Yesu. Lakini wengi duniani
hawadai wanamwamini Yesu. Lakini Mungu alionya kuwa hata miongoni mwa wanaodai kumwamini
Yesu, hata miongoni mwa wanaomwita Bwana, wengi watamwambia,
Tulifanya kazi nzuri zote hizi. Kwa nini hatukuokolewa? Atasema, Ondokeni kwangu
sikuwajua ninyi kamwe. Kwa sababu wokovu si kwa matendo. Na kama wewe
unaziamini kazi zako mwenyewe kwamba zitakuokoa, unadhani utaenda mbinguni kwa vile
umebatizwa, au wadhani, Lakini nimeishi maisha mema. Nadhani
inabidi uzishike amri ili ukokolewe. Nadhani inabidi uende kanisani. Nadhani
lazima uache dhambi kama unategemea matendo yako, Yesu
atasema siku moja, Ondoka kwangu, sikukujua kamwe. Unatakiwa
uwe na imani kwa yale aliyofanya. Uamini yale Yesu aliyafanya pale
msalabani, pale alipokufa na kuzikwa na kufufuka. Hiyo ndiyo tiketi yako ya
kwenda mbinguni. Ukiamini, Aah, nitaenda mbinguni kwa vile mimi ni mkristo
mwema, nitendaye matendo haya mema, atakuambia, Ondoka kwangu.
Sikiliza asemacho: Ondokeni kwangu, sikuwajua ninyi KAMWE. Siyo, nilikuwa nawajua
Kwa vile mara akishakutambua, kama nilivyosema mwanzo, ni kwa milele. Ni milele.
Akishakutambua, umeokolewa milele. Lakini asemapo, Ondokeni kwangu,
sikuwajua ninyi kamwe. Ukiena motoni, ni kwa sababu hakukujua kamwe. Mara akishakujua,
Anakujua. Ni kama tu vile watoto wangu siku zote watabakia kuwa ni watoto wangu. Pale
unapozaliwa mara ya pili, unapofanyika mtoto Wake, siku zote utakuwa mtoto Wake. Unaweza ukawa
chakaramu wa familia. Unaweza kuwa mtu unayeadhibiwa sana na Mungu duniani hapa.
Unaweza kuharibu maisha yako ya hapa duniani, lakini huwezi kuharibu wokovu. Umeshaokolewa.
Imekwisha kamilika. Kwa hiyo jambo kuu nililotaka kulileta kwako kuhusu
siku za mwisho. Na tumebakiwa na dakika chache
kwa maswali kuhusu ama wokovu au siku za mwisho.
Yesu utupendaye, najua mimi ni mwenye dhambi. Najua nastahili kwenda motoni,
Lakini naamini ulikufa msalabani kwa ajili yangu na ulifufuka.
Tafadhali niokoe hivi sasa na unipe uzima wa milele. Nakuamini wewe tu, Yesu. Amen.
|